KWELI Video hii ya bodaboda wanaotoa ushuhuda kuhusu barabara imetengnezwa kwa Akili Unde

KWELI Video hii ya bodaboda wanaotoa ushuhuda kuhusu barabara imetengnezwa kwa Akili Unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1

1759818708534.png
 
Tunachokijua
Katika mtandao wa TikTok kimechapishwa kipande cha video kinachowaonesha watu wenye pikipiki barabarani wakielezwa kubwa ni bodaboda wakitoa ushuhuda wao ambapo umeambatanishwa ujumbe unaosema "barabara zimejengwa, na miundombinu rafiki kuwawezesha wasafirishaji kufanya kazi yao kwa usalama siasa zetu sasa tanzania CCM"

Je, video hiyo ni halisi?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali umejiridhisha kuwa video hiyo si halisi kwani imetengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Akili Unde.

Aidha video hiyo imeambatana na mapungufu kadhaa yanyokinzana na uhalisia. Mfano licha ya kuwa ni picha mjongeo lakini wapo watu wanaoonekana wameganda pasipo kufanya kitu chochote, Uwepo wa magari yasiyotembea katikati ya barabara, kufanana kwa miondoko ya vicheko vya bodaboda hao, kukosewa kwa maneno yaliyopo katika video (Subtitles).​


1759993400278-png.3485904
Movement za vicheko zinafanana na kuendana kama wimbo wa lucky dube
 
Back
Top Bottom