POTOSHI Video hii ya RC Kihongosi akitoa adhabu ya viboko kwa watu wazima ni ya mwaka 2025?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Halafu RC wa Arusha Kihongosi yawezekana ana Uzoefu wa Kuchapa Bakora kwani si kwa Bakora za maana alizowachapa.

Your browser is not able to display this video.


 
Tunachokijua
Madai

Baadhi ya vyanzo ikiwemo The Nairobi Times kupitia ukurasa wao wa mtandao wa X wamechapisha taarifa iliyoambata na mtu anayeonekana kutoa adhabu ya viboko kwa watu wazima ofisini na kuelezwa kuwa huyo ni mkuu wa mkoa wa Arusha akitoa adhabu kwa wakandarasi waliochelewa kuleta samani za shule.

"Shock in Tanzania as Arusha Commissioner Caught on Video Whipping Contractors Over Delayed School Furniture Delivery, Watch" Chanzo hicho kiliandika

Uhalisia wa Taarifa hiyo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa Taarifa hiyo inapotosha uhalisia.

Ufuatiliaji kwa njia ya google reverse search imebainika kuwa video hiyo si ya hivi karibuni (2025) na badala yake imekuwepo mtandaoni kuanzia Disemba 2020 ambapo aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Arusha aliwaadhibu kwa viboko wanafunzi pamoja na wafanyabiashara ya vyuma chakavu ambapo vyanzo mbalimbali vilichapisha taarifa hiyo.

Mathalani chaneli ya Youtube ya Global TV, Disemba 16, 2020 ilichapisha kipande hicho cha video chenye dakika 7:48 ikiabatana na taarifa inayosomeka; DC 'AWACHARAZA' VIBOKO WAFANYABIASHARA LAIVU MBELE ya VIONGOZI wa SHULE.

Taarifa hiyo ya Global iliendelea kueleza; Mkuu wa wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi, Amewatandika viboko wanafunzi watatu na wafanyabiashara wanne wa vyuma chakavu walionunua viti vya shule na kuvifanya vyuma chakavu…

Chanzo kingine kilichoripoti tarifa hiyo ni Mwananchi Disemba 16, 2020 waliandika;

"Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi amewacharaza bakora wanafunzi watatu wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Sinoni kwa tuhuma za kuiba madawati 108 ya shule hiyo na kuyauza kama vyuma chakavu.

Wanafunzi hao wanadaiwa kuiba madawati hayo kwa nyakati tofauti na kuwauzia watu watano ambao tayari wamekamatwa na polisi.

Akizungumza leo Jumatano Desemba 16, 2020 wakati akiwaadhibu watoto hao mbele ya wazazi wao na wanafunzi, mkuu huyo wa Mkoa amesema madawati hayo yana thamani ya Sh10 milioni na kwamba watakaohusika kuhakikisha yanapatikana mengine ni walioyanunua pamoja na wazazi wa wanafunzi hao.

Mkuu wa shule hiyo, Nteles Lorna amesema walinzi wa shule walibaini wizi huyo baada ya kuona madawati yamepungua."


Jambo hilo lilizua mijadala na maoni mbalimbai na kutoka kwa wananchi na makundi mengine, tazama mjadala hapa ulivyokuwa kupitia jukwaa la JamiiForums
Halafu RC wa Arusha Kihongosi yawezekana ana Uzoefu wa Kuchapa Bakora kwani si kwa Bakora za maana alizowachapa.
Katika watu wanaoamini kuwa mtoto hulelewa na jamii na si familia yake pekee, ni watu wa Arusha. Ndo maana unaona mpaka leo wana utamaduni wa kumuadhibu mtu (kwa makundi) kwa kumchapa fimbo sabini.

Kwa hiyo RC (kumsaidia Mwalimu Mkuu) kuwachapa watoto wakosefu, hilo haliwezi kuwahangaisha hata kidogo.
 
Huyu Mkuu wa Mkoa kwa ufupi kapwaya sana
 
Aisee!!
 
Hiyo video ni ya zamani wakati mhe kihongosi ni Mkuu wa wilaya
 
Mwanaume unaogopa viboko?πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…