KWELI Video hii ya refa aliyechezesha mechi ya Morocco na Tanzania imetengezwa kwa kutumia akili unde

KWELI Video hii ya refa aliyechezesha mechi ya Morocco na Tanzania imetengezwa kwa kutumia akili unde

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kumekuwa na video ambayo inasaambaa kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook ikimuonesha aliyekuwa refree wa mchezo kati ya Morocco dhidi ya taifa stars akizungumza mara baada ya kutamatika kwa mchezo huo ambao ulisha kwa morocco kuondoka na ushindi wa goli moja kwa bila.

Mchezo huo wa raundi ya kumi na sita 16 umechezeshwa na refree kutoka mali ambaye anaitwa Boubou Traoré

1767619995907.png

 
Tunachokijua
Baada ya mechi ya mpira wa miguu ya mashindano ya mataifa barani Afrika (AFCON) kutamatika kati ya Timu ya Taifa ya Morocco na timu ya Taifa ya Tanzania hatua ya 16 bora iliyopelekea Tanzania kutolewa kumekuwa na maoni tofauti ikiwemo yale yanaeleza kuwa Refa Boubou Traore hakutenda haki kwa timu ya Tanzania.

Madai

Kumekuwa na kipande cha video kinachosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kikimuonesha refa Boubou Traore akitamka maneno yafuatayo kwa lugha ya kiswahili.

umeona inavyo uma sasa, hayo ndio maumivu ya dhuluma hayo ndiyo maumivu ya mtu anaye nyimwa haki. Imagine hiyo ni haki kwenye mpira sisi tunaonyimwa haki ya kuishi tunaumia vipi? kwanza, mnatumia pesa zetu vibaya hatuna maji jengeni.
uhalisia wa video hiyo

JamiiCheck imefuatilia kipande cha video kinachomuonesha refa wa kati aliyechezesha mechi kati ya Tanzania na Morrocco Januari 04, 2025 akieleza namna gani dhuluma inavyouma na kubaini kuwa imehaririwa kwa teknolojia ya Akili Unde (AI).

Kupitia nyenzo za kidigitali imebainika kuwa sauti hiyo inayosikika katika video hiyo imetengenezwa kwa teknolojia ya Akili Unde (AI), Nyenzo ya Deepfake total imebainisha kuna uwezekano wa zaidi ya 75% wa sauti hiyo kuwa imetengenezwa kwa AI.

1767618824169-png.3525627


Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa video hii imetengenezwa kwa kurejelea chapisho lililochapishwa na msanii Roma kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo aliandika;

Umeona inavyouma eee??

Sasa hayo ndio maumivu ya dhuluma!!
Hayo ndio maumivu anayopata mtu anayenyimwa haki!!

Imagine hiyo ni haki kwenye mpira tu inauma hivyo!!

Sisi tunaonnyimwa haki za kuishi tunaumia vipi!??

KWANZA MNATUMIA PESA ZETU VIBAYA
HATUNA MAJI……JENGENI VISIMA
1767618185902-png.3525621
Back
Top Bottom