VIDEO: Hili shangwe la Wabunge kwa Shaka Hamdu Shaka linamaanisha nini kwa Siasa za Sasa, Je arudishwe?

Mwanahabari Huria

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2025
Posts
406
Reaction score
308
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limetikiswa na shangwe na makofi kutoka kwa wabunge mara baada ya kutambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, aliyekuwa miongoni mwa wageni wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Mei 22, 2026.

Mara tu jina lake lilipotajwa ndani ya ukumbi wa Bunge, wabunge walilipuka kwa shangwe na makofi, ishara iliyoonyesha namna alivyoacha alama na kumbukumbu kwa viongozi na wananchi kupitia utendaji wake wa kazi katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama.

Akizungumza baada ya shangwe hilo, Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Najma Murtaza Giga, alisema wazi kuwa mapokezi hayo ya kipekee yanaweza kuwa yametokana na utendaji mahiri wa Shaka Hamdu Shaka kipindi alipokuwa akihudumu kama Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa.

Tukio hilo limeendelea kuvuta hisia za wengi ndani na nje ya Bunge, huku likionyesha namna viongozi wanaotumikia wananchi kwa kujituma hubaki katika mioyo ya watu hata wanapobadilika nafasi za uongozi.
 
Mheshimiwa Shaka Hamidu Shaka Ni Hazina Kubwa sana kwa Taifa letu hili la Tanzania. Ni Bonge Moja La Kiongozi. Ninamkubali sana utendaji na uchapakazi wake Tangia akiwa UVCCM Mpaka Ndani ya Chama.

Namtakia Kila lenye Heri na naendelea kumuombea sanaa Safari yenye mafanikio na Matumaini.

Ni Kiongozi Mtulivu ,mwenye Busara, Hekima ,utu, uungwana Na Moyo wa Uzalendo Na Dhamira Njema Kwa Taifa Hili.
 
Mheshimiwa Shaka Hamidu Shaka Ni Hazina Kubwa sana kwa Taifa letu hili la Tanzania. Ni Bonge Moja La Kiongozi.Ninamkubali sana utendaji na uchapakazi wake Tangia akiwa UVCCM Mpaka Ndani ya Chama .Namtakia Kila lenye Heri na naendelea kumuombea sanaa Safari yenye mafanikio na Matumaini.

Ni Kiongozi Mtulivu ,mwenye Busara,Hekima ,utu, uungwana Na Moyo wa Uzalendo Na Dhamira Njema Kwa Taifa Hili.
Umemueleza vizuri sana Shaka Hamdu Shaka
 
Shaka ni kiongozi mzuri kweli, wilaya ya kilosa amejitahidi sana.

Sema kuna sehemu kijiji kimoja bado kuna mambo magumu sana pale, kijiji cha Kwambe pale anatakiwa kupaangalia kwa umakini sana. Kile kijiji ni kama kiko gamboshi, kipo njiani kabisa hakina chochote, nilitaka ku invest pale mambo niliyokutanana nayo pale, bila kuangalia uongozi wa pale, bado.

Alifika pale lakini hakufanya maamuzi, suala la mgogoro wa maguha shaka hapo kaingizwa kingi na kajaa kwenye mfumo.

Bado hapo apambane, ila anajitaidi.
 
Huyu enzi fulani aliolewa huko Mombasa hadi Uvccm wakapendekeza afukuzwe uanachama, sidhani kama ameacha huo uchafu, na sijui huko CCM nani anamla sasa hivi.
 
Yale malalamiko ya yule mama kule kiloso kuwa anaegemea kwa wafugaji naona vyombo vy habari wameyapotezea kabisa.
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limetikiswa na shangwe na makofi kutoka kwa wabunge mara baada ya kutambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, aliyekuwa miongoni mwa wageni wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Mei 22, 2026.

Mara tu jina lake lilipotajwa ndani ya ukumbi wa Bunge, wabunge walilipuka kwa shangwe na makofi, ishara iliyoonyesha namna alivyoacha alama na kumbukumbu kwa viongozi na wananchi kupitia utendaji wake wa kazi katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama.

Akizungumza baada ya shangwe hilo, Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Najma Murtaza Giga, alisema wazi kuwa mapokezi hayo ya kipekee yanaweza kuwa yametokana na utendaji mahiri wa Shaka Hamdu Shaka kipindi alipokuwa akihudumu kama Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa.

Tukio hilo limeendelea kuvuta hisia za wengi ndani na nje ya Bunge, huku likionyesha namna viongozi wanaotumikia wananchi kwa kujituma hubaki katika mioyo ya watu hata wanapobadilika nafasi za uongozi.
Hayo yote ni mahaba ya nguchiro wa CCM kwa nguchiro mwenzao.
 
Shaka ni mpiga domo mzuri na siasa inataka watu wa hivyo.
 
Huyu jamaa alimkosea nini Maza hadi akapigwa demotion kubwa namna ile?
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limetikiswa na shangwe na makofi kutoka kwa wabunge mara baada ya kutambulishwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Shaka Hamdu Shaka, aliyekuwa miongoni mwa wageni wa Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Mei 22, 2026.

Mara tu jina lake lilipotajwa ndani ya ukumbi wa Bunge, wabunge walilipuka kwa shangwe na makofi, ishara iliyoonyesha namna alivyoacha alama na kumbukumbu kwa viongozi na wananchi kupitia utendaji wake wa kazi katika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama.

Akizungumza baada ya shangwe hilo, Mwenyekiti wa Bunge, Mhe. Najma Murtaza Giga, alisema wazi kuwa mapokezi hayo ya kipekee yanaweza kuwa yametokana na utendaji mahiri wa Shaka Hamdu Shaka kipindi alipokuwa akihudumu kama Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa.

Tukio hilo limeendelea kuvuta hisia za wengi ndani na nje ya Bunge, huku likionyesha namna viongozi wanaotumikia wananchi kwa kujituma hubaki katika mioyo ya watu hata wanapobadilika nafasi za uongozi.
Shaka mwamba sana aisee👍
 
Ukaona ujianzishie na uzi kabisa ukipewa support na ID za tumbili.
 
Back
Top Bottom