1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 7,201
- 9,529
Kumpata Rais wa nchi ni gharama kubwa kwa Taifa. Ndio maana sheria inamlinda sana na wananchi pia tunamlinda na kumpigania na kumwombea Rais wetu.View attachment 1653914
Rais John Pombe Magufuli pamoja na kuwa ni aggressive na mkali, lakini hatujawahi kumwona akishika kiboko kucharaza viboko watu hadharani...!!
Rais John Pombe Magufuli pamoja na kwamba hapendi wahalifu na matumizi mabaya ya rasrimali za nchi ikiwemo fedha, lakini hajawahi kuamuru wahujumu uchumi, watakatishaji fedha ama wezi wa mali ya umma wapigwe risasi ama viboko hadharani....
Rais John Pombe Magufuli, huponda na kufokafoka kwa maneno makali na ya kuudhi (sometimes) lakini huamuru uchunguzi kufanyika na hatua za kawaida za kikazi na kisheria kutendeka...
Huyu DC yeye ni nani hasa hata afanye ujinga kama huu? Kwa kweli simuelewi na sijui kama nitamwelewa...!
View attachment 1653943
HAPA JAMAA ANATENDA UJINGA, ANATOA HUKUMU...
Polisi wangekuwa na mtazamo na akili kama za huyu DC, basi mpaka sasa kusingekuwa watu magerezani maana wangekuwa wanahukumiwa papo hapo kwenye tukio...
Jamii hususani watoto wajifunze nini toka kwa kiongozi kama DC huyu anayejitetea kwa ujinga wa matendo yake?....
Je, jamii ijifunze na kuona kuwa kumbe ni sawa watu kujichukulia sheria mkononi kwa wanaowadhania ni "wahalifu" ama "wakosaji" kama alivyofanya DC?..
Kama mtazamo wa DC ndivyo ulivyo, kumbe basi, hakuna haja ya kuwa na mahakama Tanzania..
Baada ya kuona uhalifu huo, kila mtu angetarajia kumuona DC akiamuru watu hao anaodhani ni wahalifu wakipelekwa mahakamani, lakini looh, DC akadhani yuko juu ya sheria na kujiamulia mwenyewe adhabu ya kuwapa....!
Sijui ni kwanini huyu DC mpaka sasa bado yuko ofisini maana amekosa sifa za kuwa kiongozi ktk nafasi hiyo asilani...!!
Kumpata mbunge ni gharama kubwa pia.
.
Lakini kumteua mkuu wa Wilaya haihitaji gharama hata ukiandika majina kwenye vikaratasi na Kufanya Randomly selection anapatikana.
Hivyo kama kuna DC anayeweza kujiona kuwa yeye ni wa ghali sana basi ajue kuwa anabebwa na maamuzi ya mtu mmoja katika watu mil.60.kama
Kwa umri wa yule DC ni bora angefichwa kwa kutafutiwa kibarua kingine na sio Kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Kuwa Mwenyekiti wa Ulinzi na usalama katika Wilaya halafu anashindwa kuweka Usalama wa watu kisheria ni tatizo kubwa sana. Maamuzi ya kiutawala na kiusalama huwezi ukayarikodi na kuyaweka kwenye motandao. Kwa sababu Mkuu wa Wilaya anayoyafanya hatutegemei kuwa alikurupuka tu kutoka ofisini na kwenda kuwapiga watuhumiwa bila kujadili athari na faida ya maamuzi yale kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Labda tujaribu kujiuliza hivi Walioko kwenye ile kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kama OCD na DSO nao wakiamua kupiga watu na kujirikodi ili waonyeshe jamii na aliyewaajiri kuwa wanapiga kazi nchi itakuaje?
Kama aliamua kuwatandika viboko kama adhabu haramu si angejirikodi kisha awarushie anaoona kuwa watafurahishwa ni uhuni ule?
Kwa nini ajirikodi kisha arushe hadharani ?
Kwa nini asingewachapa ikaishia pale pale badala ya kuleta taharuki kwenye jamii?
Kama hadaharani anaweza kufanya unyama ule na kuutangaza je, ni managapi mabaya na ya kijinai anayoyafanya gizani ?
Hivi haoni kuwa amejenga uadui mkubwa sana kwa watu japo wanaweza wakavumilia lakini miaka 20 ijayo ajue wazi kuwa kuna kisasi kitamfuata nyuma mana ile picha itawekwa kwenye kumbukumbu kama zile za wakoloni waliokuwa wanawachapa Babu zetu.
Ni kweli kuwa babu zetu walikua wanachapwa kwa makosa waliyokuwa wanayafanya dhidi ya serikali za Kikoloni lakini adhabu hiyo mpaka Leo inahesabika kuwa ni adhabu ya Kihuni na kishenzi.
Nakumbuka Aliyewahi kuwa Rais wa Uganda Iddi Amin Dada aliwahi kuwalazimisha wazungu wambebe mgongoni kama kisasi kwa kwa udhalimu waliokuwa wamewatendea babu zetu wa kiafrika.
Kosa kubwa sana kwenye sheria zetu ni mauaji ya kukusudia lakini hakuna muuaji anayehukumiwa kwa mtizamo wa wanasiasa au watawala badala ya mahakama kulingana na sheria za nchi.
Nauliza :
Amechukua sheria mikononi mwake kwa kuongozwa na sheria ipi?
Imeanza lini kwa watawala kuwaadhibu watuhumiwa kwa mikono yao wenyewe?
Sidhani hata Enzi za mkoloni kuwa maArea Commissioner walikua anachapa watu kwa mikono yao ?
Je, nchi hii haina sheria za uongozi wa umma?