Video: Hivi "vetting" hufanyika kweli kabla ya uteuzi wa viongozi? msikilize Kenani Kihongosi akitetea kitendo chake cha kucharaza viboko watu...

View attachment 1653914

Rais John Pombe Magufuli pamoja na kuwa ni aggressive na mkali, lakini hatujawahi kumwona akishika kiboko kucharaza viboko watu hadharani...!!

Rais John Pombe Magufuli pamoja na kwamba hapendi wahalifu na matumizi mabaya ya rasrimali za nchi ikiwemo fedha, lakini hajawahi kuamuru wahujumu uchumi, watakatishaji fedha ama wezi wa mali ya umma wapigwe risasi ama viboko hadharani....

Rais John Pombe Magufuli, huponda na kufokafoka kwa maneno makali na ya kuudhi (sometimes) lakini huamuru uchunguzi kufanyika na hatua za kawaida za kikazi na kisheria kutendeka...

Huyu DC yeye ni nani hasa hata afanye ujinga kama huu? Kwa kweli simuelewi na sijui kama nitamwelewa...!
View attachment 1653943
HAPA JAMAA ANATENDA UJINGA, ANATOA HUKUMU...

Polisi wangekuwa na mtazamo na akili kama za huyu DC, basi mpaka sasa kusingekuwa watu magerezani maana wangekuwa wanahukumiwa papo hapo kwenye tukio...

Jamii hususani watoto wajifunze nini toka kwa kiongozi kama DC huyu anayejitetea kwa ujinga wa matendo yake?....

Je, jamii ijifunze na kuona kuwa kumbe ni sawa watu kujichukulia sheria mkononi kwa wanaowadhania ni "wahalifu" ama "wakosaji" kama alivyofanya DC?..

Kama mtazamo wa DC ndivyo ulivyo, kumbe basi, hakuna haja ya kuwa na mahakama Tanzania..

Baada ya kuona uhalifu huo, kila mtu angetarajia kumuona DC akiamuru watu hao anaodhani ni wahalifu wakipelekwa mahakamani, lakini looh, DC akadhani yuko juu ya sheria na kujiamulia mwenyewe adhabu ya kuwapa....!

Sijui ni kwanini huyu DC mpaka sasa bado yuko ofisini maana amekosa sifa za kuwa kiongozi ktk nafasi hiyo asilani...!!
Kumpata Rais wa nchi ni gharama kubwa kwa Taifa. Ndio maana sheria inamlinda sana na wananchi pia tunamlinda na kumpigania na kumwombea Rais wetu.

Kumpata mbunge ni gharama kubwa pia.
.
Lakini kumteua mkuu wa Wilaya haihitaji gharama hata ukiandika majina kwenye vikaratasi na Kufanya Randomly selection anapatikana.

Hivyo kama kuna DC anayeweza kujiona kuwa yeye ni wa ghali sana basi ajue kuwa anabebwa na maamuzi ya mtu mmoja katika watu mil.60.kama
Kwa umri wa yule DC ni bora angefichwa kwa kutafutiwa kibarua kingine na sio Kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.

Kuwa Mwenyekiti wa Ulinzi na usalama katika Wilaya halafu anashindwa kuweka Usalama wa watu kisheria ni tatizo kubwa sana. Maamuzi ya kiutawala na kiusalama huwezi ukayarikodi na kuyaweka kwenye motandao. Kwa sababu Mkuu wa Wilaya anayoyafanya hatutegemei kuwa alikurupuka tu kutoka ofisini na kwenda kuwapiga watuhumiwa bila kujadili athari na faida ya maamuzi yale kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Labda tujaribu kujiuliza hivi Walioko kwenye ile kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kama OCD na DSO nao wakiamua kupiga watu na kujirikodi ili waonyeshe jamii na aliyewaajiri kuwa wanapiga kazi nchi itakuaje?

Kama aliamua kuwatandika viboko kama adhabu haramu si angejirikodi kisha awarushie anaoona kuwa watafurahishwa ni uhuni ule?
Kwa nini ajirikodi kisha arushe hadharani ?
Kwa nini asingewachapa ikaishia pale pale badala ya kuleta taharuki kwenye jamii?
Kama hadaharani anaweza kufanya unyama ule na kuutangaza je, ni managapi mabaya na ya kijinai anayoyafanya gizani ?

Hivi haoni kuwa amejenga uadui mkubwa sana kwa watu japo wanaweza wakavumilia lakini miaka 20 ijayo ajue wazi kuwa kuna kisasi kitamfuata nyuma mana ile picha itawekwa kwenye kumbukumbu kama zile za wakoloni waliokuwa wanawachapa Babu zetu.

Ni kweli kuwa babu zetu walikua wanachapwa kwa makosa waliyokuwa wanayafanya dhidi ya serikali za Kikoloni lakini adhabu hiyo mpaka Leo inahesabika kuwa ni adhabu ya Kihuni na kishenzi.
Nakumbuka Aliyewahi kuwa Rais wa Uganda Iddi Amin Dada aliwahi kuwalazimisha wazungu wambebe mgongoni kama kisasi kwa kwa udhalimu waliokuwa wamewatendea babu zetu wa kiafrika.

Kosa kubwa sana kwenye sheria zetu ni mauaji ya kukusudia lakini hakuna muuaji anayehukumiwa kwa mtizamo wa wanasiasa au watawala badala ya mahakama kulingana na sheria za nchi.

Nauliza :
Amechukua sheria mikononi mwake kwa kuongozwa na sheria ipi?
Imeanza lini kwa watawala kuwaadhibu watuhumiwa kwa mikono yao wenyewe?
Sidhani hata Enzi za mkoloni kuwa maArea Commissioner walikua anachapa watu kwa mikono yao ?
Je, nchi hii haina sheria za uongozi wa umma?
 
Wazazi wa watoto walioshiriki huo wizi ndugu na jamaa bila ya kuombwa wameenda wenyewe shule na ofisi za serikali kuomba msamaha kwa matendo waliyofanya watoto wao.

Wazazi hao hao kabla ata awajaambiwa wameamua kuanzisha harambee kurudisha ivyo viti na madawati; mtu yeyote timamu akisikia kilichofanyika anaweza elewa hatua za mkuu wa wilaya.

Watu wamezuiwa likizo kwa sababu ya kutatua hizo changamoto za madarasa, viti na madawati; halafu watu wanaenda iba kisa chuma chakavu ni upuuzi uliopindukia.
 
Jiulize kwa nini Raisi Magufuli hajatengua uteuzi wake ? Mbona wengine hata kama ni Jumapili au sikukuu utasikia katenguliwa mara moja, maana yake ni kwamba Raisi wa nchi mwenyewe angefanya hivyo hivyo, huyo DC mnamuonea tu lkn aliyewachapa viboko hao Watanzania ni Raisi Magufuli mwenyewe, so sad, unapokuwa na Raisi wa nchi ambaye kwa kawaida anapaswa kulinda na kuwatetea Wananchi yeye ndiye wa kwanza kuonea, kudhalilisha mtu mweusi, Raisi Magufuli atashindwa na hatofanikiwa kama anaonea Watanzania, Mungu atamlaani na kumuadhibu.

Mahakama peke yake ndiyo inayopaswa kuhukumu, kama hao Watanzania walifanya makosa kuna polisi, wangewakamata na kuwafikisha Mahakamani na hukumu kutolewa kwa mujibu wa Sheria zetu, ...
Kama siamini nilichosoma! Hapana. Iko hivi: kilichoandikwa ni lulu lakini mdomoni mwa nguruwe! Kama kuna muungwana kaiba ID na kuandika tuyasomayo. Ndoto gani tena hii. Barbarosa style ya kufungia mwaka. Kaokoka lini? Hii ni ndoto!
 
Hizo adhabu alizochukua DC ni hatua za awali kama mzazi.Tunafuga watoto wapumba.vu sana! DC yuko sahihi sana kwa watoto wapumb.avu kama hao.
 
Kama swala ni wizi hiyo ni kazi ya polisi sasa sijui DC katoka wapi na mambo hayo ambayo yalipaswa kushughulikiwa na Polisi.

Watu wengine wanakipa shida Chama kujieleza mbele za wananchi.
Barbarosa kaokoka na Stroke hana kile kiharusi chake tena! Tunafunga mwaka vizuri.
 
Kama swala ni wizi hiyo ni kazi ya polisi sasa sijui DC katoka wapi na mambo hayo ambayo yalipaswa kushughulikiwa na Polisi.

Watu wengine wanakipa shida Chama kujieleza mbele za wananchi.
Anashindwa kuelewa kuwa Jamii haina tatizo na wezi kuadhibiwa ila wanahoji mamlaka yake kutoa hiyo adhabu ameyapata kwa taratibu zipi.

Kwann asitokee mwandishi wa kumuuliza kama kuna umuhimu wa kuendelea na utaratibu wa kupeleka wezi mahakamani na kama upo umuhimu ni kwanini hakuufata?
 
Hizo adhabu alizochukua DC ni hatua za awali kama mzazi.Tunafuga watoto wapumba.vu sana! DC yuko sahihi sana kwa watoto wapumb.avu kama hao.
Twanga mpumbavu kinuni kwa mchi wa chuma bado atatoka na upumbavuwe! Barbarosa kaokoka, Stroke kapona lakini Funzadili shiiida tu.
 
Wazazi wa watoto walioshiriki huo wizi ndugu na jamaa bila ya kuombwa wameenda wenyewe shule na ofisi za serikali kuomba msamaha kwa matendo waliyofanya watoto wao.

Wazazi hao hao kabla ata awajaambiwa wameamua kuanzisha harambee kurudisha ivyo viti na madawati; mtu yeyote timamu akisikia kilichofanyika anaweza elewa hatua za mkuu wa wilaya.

Watu wamezuiwa likizo kwa sababu ya kutatua hizo changamoto za madarasa, viti na madawati; halafu watu wanaenda iba kisa chuma chakavu ni upuuzi uliopindukia.
Ukifanya ubakaji kwa mwanafunzi ukampa ujauzito, wazazi wake wakakufata na kwa ridhaa yao wakakupa binti yao umuoe na wewe ukamuoa, kunahalalisha ubakaji ulioufanya?

DC hakufata taratibu na sheria zetu za adhabu kwa wezi, tunazo sheria na utaratibu wa kuadhibu wezi.
Kutokuzifuata hizo sheria hakuhalalishwi na baadhi ya wanajamii kukubaliana na ulilolitenda kwa kuja ofisii kwako au kulipa fidia au kukupongeza kwa namna yoyote.

Kama hufuati sheria wewe ni mvunja sheria hata kama ukipongezwa na zawadi ukapewa kwa kuvunja hizo sheria.

Wale wezi wanatakiwa waadhibiwe, tena adhabu kali ili iwe fundisho ila adhabu zitoke kwa mamlaka husika na kwa taratibu zilizopo.

KUNA BINADAMU MPAKA WAONE MAMA, BABA, BINTI, MWANA WAKE AKITANDIKWA VIBOKO NDIO ATALAANI, KINYUME NA HAPO ATAONA NI SAWA TU.
 
View attachment 1653914

Rais John Pombe Magufuli pamoja na kuwa ni aggressive na mkali, lakini hatujawahi kumwona akishika kiboko kucharaza viboko watu hadharani...!!

Rais John Pombe Magufuli pamoja na kwamba hapendi wahalifu na matumizi mabaya ya rasrimali za nchi ikiwemo fedha, lakini hajawahi kuamuru wahujumu uchumi, watakatishaji fedha ama wezi wa mali ya umma wapigwe risasi ama viboko hadharani....

Rais John Pombe Magufuli, huponda na kufokafoka kwa maneno makali na ya kuudhi (sometimes) lakini huamuru uchunguzi kufanyika na hatua za kawaida za kikazi na kisheria kutendeka...

Huyu DC yeye ni nani hasa hata afanye ujinga kama huu? Kwa kweli simuelewi na sijui kama nitamwelewa...!
View attachment 1653943
HAPA JAMAA ANATENDA UJINGA, ANATOA HUKUMU...

Polisi wangekuwa na mtazamo na akili kama za huyu DC, basi mpaka sasa kusingekuwa watu magerezani maana wangekuwa wanahukumiwa papo hapo kwenye tukio...

Jamii hususani watoto wajifunze nini toka kwa kiongozi kama DC huyu anayejitetea kwa ujinga wa matendo yake?....

Je, jamii ijifunze na kuona kuwa kumbe ni sawa watu kujichukulia sheria mkononi kwa wanaowadhania ni "wahalifu" ama "wakosaji" kama alivyofanya DC?..

Kama mtazamo wa DC ndivyo ulivyo, kumbe basi, hakuna haja ya kuwa na mahakama Tanzania..

Baada ya kuona uhalifu huo, kila mtu angetarajia kumuona DC akiamuru watu hao anaodhani ni wahalifu wakipelekwa mahakamani, lakini looh, DC akadhani yuko juu ya sheria na kujiamulia mwenyewe adhabu ya kuwapa....!

Sijui ni kwanini huyu DC mpaka sasa bado yuko ofisini maana amekosa sifa za kuwa kiongozi ktk nafasi hiyo asilani...!!

Watanzania tuacheni unafiki. Mtu akiiba mali ya umma tunataka asipigwe hata kofi, lakini akituibia mali zetu binafsi tunakuwa wa kwanza kumvisha matairi, kummwagia mafuta na kumchoma moto. Utter nonsense! Na huu utamaduni wa kutothamini mali ya umma kama tunavyothamini mali zetu binafsi ndio ulioliweka taifa letu kwenye hadhi ya shamba la bibi!

We cannot afford to pretend to be at a civilization stage that we, obviously, haven’t attained yet!
 
Sina hakika hata kama unajua unaandika nini...

Kwa sababu hii tabia unayoitetea ya wananchi kujichukulia sheria mkononi ndiyo hiyo hiyo viongozi wanaipinga na kujaribu kuwaelimisha wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake wakikamata mwizi au mhalifu yeyote, wanashauriwa kumpeleka kwenye vyombo vya sheria...

Lakini wewe na DC wako huyu ni kana kwamba hamjui hili na hamjui sheria inasemaje...!
 
Wazazi wa watoto walioshiriki huo wizi ndugu na jamaa bila ya kuombwa wameenda wenyewe shule na ofisi za serikali kuomba msamaha kwa matendo waliyofanya watoto wao.

Wazazi hao hao kabla ata awajaambiwa wameamua kuanzisha harambee kurudisha ivyo viti na madawati; mtu yeyote timamu akisikia kilichofanyika anaweza elewa hatua za mkuu wa wilaya.

Watu wamezuiwa likizo kwa sababu ya kutatua hizo changamoto za madarasa, viti na madawati; halafu watu wanaenda iba kisa chuma chakavu ni upuuzi uliopindukia.
Wewe sijui unashindwa kuelewa kitu gani ktk mjadala huu...

Hakuna mtu anayepinga wala kutetea wezi na waharibifu wa Mali za umma ama za watu wengine...

Tunachojadiliana hapa na kuona hakifai ni watu kutofuata sheria ktk kushughulika na wahalifu ama wezi ama waharibifu wa mali za umma...

Mbona kuna viongozi wengi tu wakubwa na wenye vyeo vya juu wanatenda makosa makubwa makubwa ya ufisadi, rushwa, wizi, ulawiti, kila aina ya jinai nk nk...?

Je, ina maana hawa nao jamii ijichukulie sheria mkononi kuwavamia kwenye majumba na ofisi zao kuwaadhibu? Tutakuwa jamii ya namna gani hiyo isiyokuwa na utaratibu?

Wote tunafahamu kuwa chombo pekee kinachomtia mtu hatiani na kumpa adhabu yoyote ikiwemo ya viboko ni mahakama. Huyu DC yeye ni nani?

Unasema familia za waliotenda uhalifu huo wamelipa na kuomba msamaha. Kama wako intimidated unategemea wafanye nini? Defenetely, lazima watishike na wafanye jambo lolote so long as waepukane na adhabu ya DC na watu wake...!!
 
Haiwezekani kupanda ngano uvune karanga.
Wanaofanya hiyo vetting ni watu wa aina gani?
Yawezekana unategemea tembo ale nyama.
 
Ukifanya ubakaji kwa mwanafunzi ukampa ujauzito, wazazi wake wakakufata na kwa ridhaa yao wakakupa binti yao umuoe na wewe ukamuoa, kunahalalisha ubakaji ulioufanya?

DC hakufata taratibu na sheria zetu za adhabu kwa wezi, tunazo sheria na utaratibu wa kuadhibu wezi.
Kutokuzifuata hizo sheria hakuhalalishwi na baadhi ya wanajamii kukubaliana na ulilolitenda kwa kuja ofisii kwako au kulipa fidia au kukupongeza kwa namna yoyote.

Kama hufuati sheria wewe ni mvunja sheria hata kama ukipongezwa na zawadi ukapewa kwa kuvunja hizo sheria.

Wale wezi wanatakiwa waadhibiwe, tena adhabu kali ili iwe fundisho ila adhabu zitoke kwa mamlaka husika na kwa taratibu zilizopo.

KUNA BINADAMU MPAKA WAONE MAMA, BABA, BINTI, MWANA WAKE AKITANDIKWA VIBOKO NDIO ATALAANI, KINYUME NA HAPO ATAONA NI SAWA TU.
Wewe sijui unashindwa kuelewa kitu gani ktk mjadala huu...

Hakuna mtu anayepinga wala kutetea wezi na waharibifu wa Mali za umma ama za watu wengine...

Tunachojadiliana hapa na kuona hakifai ni watu kutofuata sheria ktk kushughulika na wahalifu ama wezi ama waharibifu wa mali za umma...

Mbona kuna viongozi wengi tu wakubwa na wenye vyeo vya juu wanatenda makosa makubwa makubwa ya ufisadi, rushwa, wizi, ulawiti, kila aina ya jinai nk nk...?

Je, ina maana hawa nao jamii ijichukulie sheria mkononi kuwavamia kwenye majumba na ofisi zao kuwaadhibu? Tutakuwa jamii ya namna gani hiyo isiyokuwa na utaratibu?

Wote tunafahamu kuwa chombo pekee kinachomtia mtu hatiani na kumpa adhabu yoyote ikiwemo ya viboko ni mahakama. Huyu DC yeye ni nani?

Unasema familia za waliotenda uhalifu huo wamelipa na kuomba msamaha. Kama wako intimidated unategemea wafanye nini? Defenetely, lazima watishike na wafanye jambo lolote so long as waepukane na adhabu ya DC na watu wake...!!
You are missing the point ya kitendo cha kuchapwa. Fimbo sio substitute ya adhabu ya mahakama, isipokuwa kuna makosa mengine yanaathiri jamii ndio kinachokera.

Ntakupa mfano ata huko tunapotaka kukopi kila kitu mfungwa anaeingia jela kwa kosa la kubaka watoto wadogo, kuuwa watoto wadogo au wazee; adhabu yake ya maisha atumikii na wafungwa wengine, kwanini?

Akiingia jela na majambazi ya kawaida yanayopora tu kwa silaha lakini hayana tabia ya kuuwa most likely achukui muda na mwenyewe wanamuua (kwa sababu it’s immoral for reasonable person to attack defenceless ppl kwenye utamaduni wao) ndio sababu wauaji wengi sana wa kesi zinazoigusa jamii jela uwekwa mbali na wahalifu wengine.

Ndio kama hao jamaa shida sio kuiba tu bali na upuuzi wa tendo lenyewe. Ni sawa na mpo jangwani ( desert) mnaletewa maji kwa week mara moja kwa matumizi ya kunywa. Halafu kati yenu anatokea mtu anaenda chafua kisima, au anachukua maji anaenda kuogea katikati ya week mnajukuta mmeishiwa.

Shida hapo inakuwa sio kosa tu, bali na ujinga wa kosa lenyewe ndio kilichopelekea DC kuamua kuwacharaza bakora.

Hata hao wazazi hakuna aliewatuma kwenda popote ila wameona athari za ujinga wa tendo lenyewe na namna linavyotia aibu mpaka kuamua kwenda kuomba msamaha kwa niaba ya watoto wao na kuchangishana walipe.

Mimi sishabikii viongozi kuchukua hatua mkononi; ila kuna upuuzi mwingine unakera kwakweli.
 
Sina hakika hata kama unajua unaandika nini...

Kwa sababu hii tabia unayoitetea ya wananchi kujichukulia sheria mkononi ndiyo hiyo hiyo viongozi wanaipinga na kujaribu kuwaelimisha wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi badala yake wakikamata mwizi au mhalifu yeyote, wanashauriwa kumpeleka kwenye vyombo vya sheria...

Lakini wewe na DC wako huyu ni kana kwamba hamjui hili na hamjui sheria inasemaje...!

Your argument is built around fantasies; we’re talking about real life here!

Wewe unadhani viongozi tulionao wanatoka kwenye jamii gani? Society hiyo hiyo ambayo bado inachoma moto suspected thieves ndiyo inayotoa viongozi tulionao. If anything, the whole society has to gradually evolve into that highly civilized society you’re fantasizing about.

At least the DC didn’t set the suspected thieves on fire like you hypocrites would typically do, even if only a bicycle has been stolen from you. Kama mali binafsi inakuuma, lazima mali ya umma ikuume vile vile. Otherwise, huo ni unafiki kwa kwenda mbele!

Last but not least, acheni kukariri. Sio kila disciplinary action lazima ichukuliwe na mahakama. Watu wenye authority kwenye society wanao uwezo wa kuchukua disciplinary actions ndogo ndogo!
 
Mleta mada ni aina ya wale wazazi ambaye mtoto wake akifanya kosa, yeye ana muadhibu kwa kumnyima juisi.

Kuna muda tupelekane kibandidu tu Hili discipline iwepo.....pumbavvu

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Na aliyeiba nyumba za serikali na kugwia mahawara kama njugu? Aliyenunua kivuko kibovu? ALIYEIBA RAMBIRAMBI BILA AIBU MCHANA KWEUPEEE?

Sidhani kama mleta mada alikusudia kuwakaribisha wenye majungu kuleta majungu yao hapa!
 
Back
Top Bottom