Ushauri wa bure: Kutamka sahihi majina ya watu, hasa wakuu wa nchi ni kielelezo kikubwa cha jinsi ya elimu yako ya yanayojiri duniani, jinsi unavyowaheshimu au kuwajali na jinsi ulivyo serious. Hapa Waziri wetu wa Mambo ya nchi za Nje anamtamka rais wa Misri "Ali Alsis' jina ambalo ni tofauti kabisaa na linavyoandikwa na kutamkwa. Kweli, kama kiongozi wa dilomasia huwezi kuchukua dakika kumi ukasikiliza linavyotamkwa? Tena siku hizi hata kwenye Google wanakupa matamshi. Ni kwa sababu hiyo hiyo walimpotosha rais naye akalitamka ' Al-sis' badala ya 'As siisi', nikaona midomo ya baadhi ya Mawaziri wa Misri ina 'pout' kwa kumsikia mgeni anashindwa kutamka jina la mwenyeji wake! Kama Waziri wa Mambo ya nchi za Nje lazima utamke sahihi majina ya viongozi unaokutana nao au anaokutanan nao rais, no excuses!
Halafu Misri siyo kama Comoro kuwa rais wake hajulikani. Ni nchi ambayo kila siku iko katika vyombo vya habari duniani.
Watanzania tuna tabia iliyojikita ya kuchukulia kila kitu kuwa kawaida tu, noma, bila kujiandaa au kujiandaa dakika ya mwisho. Ndiyo maana hatuendi popote!