The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,967
- 4,267
➡ CCM kwa kutumia vyombo vya dola polisi & TISS na watumishi wa umma i.e, wamesaidiwa kunyakua madaraka mikononi mwa wananchi kwa kilichoitwa "uchaguzi" lakini huu haustahili kuitwa uchaguzi bali "operesheni nyakua madaraka"
➡ Huu haukuwa uchaguzi bali operesheni nyakua madaraka ikifanywa na TISS, polisi, Wakurugenzi wa Halmashauri za majiji, manispaa, wilaya na miji kwa kuwatumia watendaji wa kata, vijiji na mitaa, watumishi wa umma hususani walimu kwa ajili ya CCM...
➡ Mtu anaweza kujiuliza swali hili: Hivi CCM, chama cha siasa kimepatwa na nini kiasi cha kuogopa uchaguzi na kuwaogopa wananchi huku kikiwa madarakani miaka zaidi ya 63? Je, hawana cha kuwaonesha wananchi ili waendelee kuungwa mkono kwa ushawishi wa kisiasa ndani ya sanduku la kura? Bila shaka CCM iko kinadharia tu lakini kiuhalisia haipo ilishakufa siku nyingi...!
➡ Ndani ya video hii, utamwona mwenyekiti wa CCM na Rais Samia Suluhu Hassan akiwa amejaa wasiwasI, hofu na woga wa kushindwa mbele ya wanajeshi (JWTZ) na kuwapa maagizo kuwa tayari wakati wowote kwa litakolotokea ktk chaguzi huu wa 2024 na ule wa mwakani 2025...