Video: Huyu kama ni mkeo utamfanyaje?

Sasa kitu gani kimekuchekesha?

Nakuelewa, nakumbuka wakati mtoto wa watu sijaanza tabia mbaya ( nilikua Jesus boy hadi watu wanatilia shaka kama nipo sawa) nikapata girlfriend analazimisha tupige kazi kabla ya ndoa. Nilikua nashangaa sana. Sasa nikaja kujua alikua akiishi na mwanaume mwingine wakati amekuja likizo ndio anataka aniingize mkenge nimuoe...nilitaka kuwa kichaa. Sikujali wazee walishaenda kujitambulisha na sikuwahi kuongelea tena muafaka wa hilo jambo hadi Sasa.

Baadae nikaja kuwaambia wakatoe mahari Kwa Mke niliyenae sasa.

Cha ajabu huyo Binti aliyetaka kunipa ukichaa leo kanitumia sms kunijulia hali. Nimejikuta naongea peke yangu.

Wivu wa mtu anaejitunza au kumpenda sana mtu hauelezeki.

Bila shaka uko salama!
 
Kama hadi kurekodi kaweza tena maeneo tofauti tofauti anamfuata ni dhahiri anajua huyo mama aezi fanya kitu na hilo panga Mkuu.

Lakini yote kwa yote huyo jamaa kazingua.
Kweli kazingua, ila kuna wanawake wengine ni wastaarabu mpaka unashangaa. Kuna jamaa yetu alitualika kwenda kwake kula mbuzi choma siku ya Kumamosi (ilikuwa ni kawaida yetu). Huwa tunaanza na mchemsho wa nguvu, then vinywaji vikali tukiwa tunasubiria nyama choma.
Tunafika pale mida ya saa tano asubuhi tunakuta hali ya usalama ishachafuka. Kumbe asubuhi mke wake kaenda sokoni kununua viungo na mahitaji mengine, huku nyuma kamuacha jamaa na shemeji yake (rafiki ya mke wake) na vijana waliokuwa wanasaidia kuchinja na kuandaa nyama.

Jamaa kumbe kaachiwa gepu na hapo tayari walishaanza konyagi asubuhi na huyo shemeji mtu, wale vijana wachinjaji wanawachora tu (kumbuka mke ndiye aliwaomba waje kusaidia). Muda si mrefu jamaa na shemeji wakapelekana chumbani, madogo wakampigia mwanamke simu fasta akageuza na kupaki gari mbali kidogo. Anaingia anamkuta mme wake anapiga mashine (chumba cha wageni) na mlango wamerudishia tu.

Yule mwanamke kwa kusaidiana na wale vijana wakawafungia watuhumiwa mle ndani, tunafika pale jamaa kawa mpole kama sisimizi, nyama haikulika tena, tulibeba tu mikonyagi tukaondoka. Mpaka leo bado ni wanandoa na wanaishi kwa furaha tele, jamaa hata pombe akapumzika kabisa na kuwa mtu wa familia kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…