Nchi yetu hii na wanaopenda kujiita wanasiasa,... sijui kama unaweza ukawapata wanasiasa kwelikweli wanaoamini na kusimamia chochote zaidi ya uanasiasa wao.
Kama wapo, basi hawajitambulishi ili tuwahesabu.
Labda, nasema labda, (kwa sababu kuna waigizaji wazuri kama yule Binti Halima Mdee); kama Mchungaji Msigwa sio muigizaji mzuri, kwa leo hii ndiye ninayeweza kusema ni tofauti. Lakini sijui.
Nyarandu aliigiza vizuri vya kutosha: alipoukosa uwaziri, halafu Magufuli kafanya aliyofanya..., ilikuwa ni uigizaji mzuri kiasi cha kutosha kwa Nyalandu kukoga nyoyo za watu kwa kuacha maslahi ya ubunge. Ni nani asingehadaika na kitendo cha namna hiyo kwa wanasiasa wetu wa siku hizi!
Siku hizi mtu kujiuzuru toka sehemu yoyote ya maslahi kwake eti kwa kulinda anayoyasimamia au kuyaamini, jambo la namna hiyo halipo kabisa.
Kwa hiyo Nyalandu, kama wenzake wote walivyo, ni msaka fursa popote anapodhani fursa inapatikana. CCM sasa hivi ndipo anapoona fursa inapatikana, kwa nini aendelee kupoteza muda wake CHADEMA!