- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu, Je hii video inayoonesha jeshi la Marekani likiwa pamoja na helcopter ni ya siku ambayo walienda kumkamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro?
- Tunachokijua
- Nicolás Maduro amekuwa Rais wa Venezuela kuanzia mwaka 2013 hadi alipokuja kutolewa baada ya kukamatwa na vikosi vya Marekani Januari 2026.
Madai
Mara baada ya Rais wa Marekani kutangaza kuwa vikosi vya taifa lake vimemkamata Rais Nicolás Maduro pamoja na mkewe, kumekuwa na kipande cha video kinachoonesha kikosi cha wananjeshi kikiwa na helkopta kwenye moja ya ghorofa na kuelezwa kuwa ni video wakati Rais Maduro anakamatwa Januari 03, 2026.
Uhalisia wa video hiyo ni upi?
JamiiCheck kwa kutumia nyenzo za kidigitali imejirirdhisha kuwa video hiyo ni halisi lakini si ya januari 03, 2026 wakati Rais Maduro wanakamatwa kama inavyoidaiwa.
Ufuatiliaji umebaini kuwa video hiyo ni ya mwezi Juni, 2025 wakati Rais wa Marekani alipokwenda kuwahutubia wanajeshi wa Marekani kuelekea maadhimisho ya miaka 250 ya jeshi hilo. Video hiyo ni moja ya maonesho ambayo Rais Trump aliyashuhudia kutoka kwa jeshi la nchi hiyo.
Hata hivyo jeshi la Marekani liliivamia Venezuelea na kumchukua Maduro majira ya usiku na picha nyingi za siku husika ni za usiku na si mchana kama inavyoonekana kwenye video inayosambazwa mitandaoni na kudaiwa ni ya Januari, 2026.