Mangekimambi: Mgonjwa wenu huyo, December 20 2017 aliposti hii video anakata mauno. Rayvanny akarepost kwake.
Alivyoanza kulia mguu unamuuma akaifuta hii video fastaaaaa ili watu wasione kuwa wiki moja tu iliyopita kabla hajaanza kulia mguu alikuwa mzima anakata mauno ila ndo hivyo Rayvanny hakuifuta kwake.
Sasa naombeni mjiulize tu jamani, Dec 20 mtu alikuwa anakatika hivi mguu haumii wiki moja baadae anaomba msaada wa kwenda India anasema mguu unatoa nyama anateseka, akasema na mgongo unamuuma mpaka anazimia, huyu ni mgonjwa wa mgongo jamani??? au mgongo ulimuanza baada ya kucheza Makulusa?? . Tena kwenye hii video aliweka na caption ‘Natafuta jasho nikaoge’
Mnaoniona nna roho mbaya acheni ujinga nyinyi, ningekuwa na roho mbaya ningemwaribia kabla hajapokea senti nimesubiri pesa imetimia ndio nimeongea, it means sina tatizo na yeye kupokea pesa tatizo ni kwamba inabidi ukweli usemwe!! Mnishukuru nilikaaa kimya kama sipo mpaka mlipoingia mkenge wote na Rais wenu .
Watu wake wa karibu wameni contact mmoja ni daktari kabisa, wameniambia tatizo alilonalo Wastara ni tatizo very normal kwa waliokatwa mguu, na hilo tatizo ni kwamba Wastara kanenepa sana so mguu wa bandia umekuwa mdogo kwa hiyo akiuvaa Muda mrefu unamchubua mguu na kumpa matatizo mengine, ila mguu wake hauna tatizo kabisaaa, tatizo ni mguu wa bandia only, kinachotakiwa ni kubadilishiwa mguu tu, hata huko India hatofanyiwa operation wala kitu chochote zaidi ya kupewa mguu mpya kitu ambacho hata hapo muhimbili wangemfanyia. Na nimeambiwa mguu wa bandia India ni between dollar 300-500 kwa watu wa kawaida. So wastara atanunua mguu mpya India atafanyia mazoezi basi.Hana complication yoyote ya kumpeleka India na yeye Wastara anajua fika kuwa anachohitaji ni anahitaji mguu mpya tu.
UPDATE
Baada ya mimi kuiposti hii video na kusema aliifuta basi Wastara kairudisha video hewani fastaaaAlikuwa kaiweka kwenye archive. Wastara bana, leo utahangaika sana. Acha utapeli! Hizo pesa ulizopata fanya biashara ya maana achana na Viben10 maana ndo hutochangiwa