Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
Jeshi la Maji la Uingereza limefanya majaribio ya kutumia mavazi maalum yanayomwezesha mtu kupaa kwa lengo la kuboresha operesheni za kuzuia uharamia baharini.
Kampuni ya utafiti wa teknolojia ya anga ya Gravity Industries imechapisha video inayoonesha wanajeshi hao wakifanya mazoezi kwa kutumia teknolojia hiyo mpya katika meli ya kivita ya HMS Tamar ya Uingereza.
Wanajeshi hao walifanya mazoezi ya kupanda meli, kufanya ukaguzi na kumkamata adui (ama VBSS) kutokea kwenye boti ya mwendokasi iliyokuwa ikiifuatilia meli hiyo, ambapo wanajeshi hao walitumia teknolojia ya kupaa kwa kutumia mavazi hayo maalum.
Kampuni hiyo imesema Makomando 42 wa Jeshi la Maji walishiriki katika operesheni hiyo kwa muda wa siku 3, operesheni inayotajwa kuwa ya hatari zaidi kwa Jeshi la Maji.
Hata hivyo, Jeshi halijaeleza ikiwa itanunua teknolojia hiyo. Teknolojia hiyo imewahi kutumiwa na wahudumu wa dharura kuwaokoa watu walio katika mazingira ya hatari, na inatajwa kusaidia kuokoa muda ambao ungetumika kuwafikia kwa miguu au kwa gari.
Teknolojia hiyo bado ipo kwenye hatua ya majaribio, na inatajwa na Kitabu cha Kumbukumbu cha Guiness kuwa ndiyo teknolojia inayoshikilia rekodi ya kuwa na kasi zaidi kwa mavazi maalum yanayovaliwa inayomwezesha mwanadamu kupaa, ikifikia maili 85 kwa saa (kilometa 136.8) katika majaribio mwaka 2019.
Chanzo: Business Insider