Video: Kenyans scramble to buy cheap unga in a supermarket.

Mzungu aliwaletea Ugali ili muwe Wajinga, Ugali mnaokula huo mweupe hauna virutubisho vyovyote vile, kwa kifupi mnakula pumba tu, mpaka a Muzungu aje tena kuwaambia mle vyakula vingine!

Wewe mbona huwa una mahaba na wazungu kiasi hiki, sijui kipi walikutendea hadi uwapende kwa moyo wote kiasi kwamba lazima uwahusishe katika kila bango zako.

Ugali unapendwa Afrika, binafsi napenda sana kula ugali, haipiti siku bila mimi kutia saini kwenye huo mlo tuupendao, na ikipita nahisi ovyo.
Japo pia inategemea na asili ya mtu, kwa mfano Pwani za Kenya na Tanzania wao wamekita kwenye kula ubwabwa, lakini ukiingia mikoani Kenya na hata kwenu huko Kolominje kwa Wasukuma, ugali unaliwa kila siku.
Ugali unaliwa hadi Afrika Kusini ambapo wanaita 'phuthu', Botswana wanaita 'bogobe', nao Zimbabwe wanaita 'sadza'
Huu mlo unatumika kwenye matatifa mbali mbali japo wanatumia majina tofauti, hayo ni mataifa kama Zambia, Malawi, Mozambique, Namibia n.k.

Rais Uhuru awaze upya na ajipange, maana kama anataka kudumisha urais ahakikishe ugali tunaupata kiulaini bila mahangaiko. Hapa Raila atavizia na kama anajua kucheza game zake vizuri aongee kuhusu ugali na unga na kuahidi Wakenya watapata unga hadi wachoke wakati yeye akiwa rais.
 
Hmm! Nilikuwa najaribu kujiuliza, hivi hii habari ya njaa Kenya kwanini ije wakati huu wa uchaguzi? I can smell something fishy here...
 
Poleni sana
Na Bongo MZEE Magu kafunga kutoa chakula nje
Kazi mnayo
 
dah! this is one of the failures of the jubilee administration...food security...hivi watanzania si mtusaidie na mahindi jameni...jamaa hapa haswa wale wa magharibi ya kenya wanahangaika kwel kwel...😀😀😀
Cc MOTOCHINI
 
Unaweza kula ugali mwaka mzima usibadili na life kwenda vizuri tu
Kuliko hivyo vyakula unavyo taja
 


Ugali wa Mahindi siyo asili ya Afrika, alileta Mzungu ktk the Americas, asili ya Afrika ni Mtama, Mihogo, n.k. kwanza Mahindi ni chakula cha Mifugo kwa Wazungu!
 
Ugali wa Mahindi siyo asili ya Afrika, alileta Mzungu ktk the Americas, asili ya Afrika ni Mtama, Mihogo, n.k. kwanza Mahindi ni chakula cha Mifugo kwa Wazungu!
Usidharau mahindi hivyo ati ni chakula cha mifugo uzunguni. Pia ni chakula cha binadamu, na wazungu pia hula vyakula vitokanavyo na mahindi: porridge, cornflakes (mostly for breakfast), cakes, fried meat and fish coated in corn flour, soup thickeners, corn syrup ( ni tamu kama sukari), beer, roasted corn nk.

Lakini nakubaliana na wewe ya kwamba hiki si asili ya waafrika, so are the most other foods, kama potatoes, yams, wheat, cassava, beans nk.
 
Wakat huo hata unga wa 90
Unamshinda kuwafkishia wananchi
Mambo kama haya hutokea katika siasa....ni mambo ya kupita,mchagueni Uhuru...ningekuwa Mkenya ningemchagua Uhuru
 
Waafrika bhana, yaani utaacha kumchagua MTU kisa huna ugali wa kula! Au utamchagua MTU kisa kakupa unga wa ugali !!!kweliii????
Yesu rudi uokoe hii ngozi nyeusi ..
Yesu akae huko huko kwanza mpaka waTIZII walipwe makinikia yao!!
 

Hicho kiini cha njano huondolewa ili ule unga uwe na longer shelf life. Mahindi yakisagwa na kuwekwa kwenye pakiti, haiwezi kudumu kwa mda mrefu, kwasabu hiyo yellow part, kwa kimombo huitwa "germ", ina mafuta na unyevunyevu inayoweza kuozesha unga na kuifanya iwe sumu kwa binadamu. Hiyo sumu huitwa "aflatoxin", na ni hatari sana; huua.

Lakini hiyo sehemu nyeupe inaitwa "endosperm" ina virutubisho sawa tu na mchele ama hayo nafaka mengine. Lakini ni kweli ya kwamba mahindi yakiondolewa hicho kiini cha manjano, hupoteza virutubisho muhimu, lakini hilo kinafidiwa kwa kula mahindi na vyakula vingine vyenye virutubisho hivyo hivyo, kama nyama na mboga au maziwa.

The germ hutumiwa Kenya kutengeza mafuta ya kupikia na some food additives, hasa zile za keki.

Kwa hivyo, usidhani wakenya wanapoteza hivi virutubisho juu ya maize germ kuondolewa.

Ugali wa mahindi meupe hayawezi kuwa manjano hata kama kiini manjano kisipoondolewa, unless umetumia yale aina ya mahindi ya manjano ambayo hayakuwi vyema huku Kenya.
 
Thats why many Kenyans are fat, and out of shape, Ugali huwa na a lot of calories. But people can eat other things na walale

Wazungu are fatter than Kenyans.
 

Wabantu na Wanailoti wote wanakula ugali, kwa ufupi Afrika nzima ukiondoa Kaskazini kwa Waarabu na pembe ya Afrika kwa Wasomali na Waethiopia.

Afrika Magharibi wanaita ugali majina kama fufu, mana na gari.
 
Hee basi kama ndo hivo watulie njaa iwashughulikie had wajifunze kula light food.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…