MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Mzungu aliwaletea Ugali ili muwe Wajinga, Ugali mnaokula huo mweupe hauna virutubisho vyovyote vile, kwa kifupi mnakula pumba tu, mpaka a Muzungu aje tena kuwaambia mle vyakula vingine!
Wewe mbona huwa una mahaba na wazungu kiasi hiki, sijui kipi walikutendea hadi uwapende kwa moyo wote kiasi kwamba lazima uwahusishe katika kila bango zako.
Ugali unapendwa Afrika, binafsi napenda sana kula ugali, haipiti siku bila mimi kutia saini kwenye huo mlo tuupendao, na ikipita nahisi ovyo.
Japo pia inategemea na asili ya mtu, kwa mfano Pwani za Kenya na Tanzania wao wamekita kwenye kula ubwabwa, lakini ukiingia mikoani Kenya na hata kwenu huko Kolominje kwa Wasukuma, ugali unaliwa kila siku.
Ugali unaliwa hadi Afrika Kusini ambapo wanaita 'phuthu', Botswana wanaita 'bogobe', nao Zimbabwe wanaita 'sadza'
Huu mlo unatumika kwenye matatifa mbali mbali japo wanatumia majina tofauti, hayo ni mataifa kama Zambia, Malawi, Mozambique, Namibia n.k.
Rais Uhuru awaze upya na ajipange, maana kama anataka kudumisha urais ahakikishe ugali tunaupata kiulaini bila mahangaiko. Hapa Raila atavizia na kama anajua kucheza game zake vizuri aongee kuhusu ugali na unga na kuahidi Wakenya watapata unga hadi wachoke wakati yeye akiwa rais.