SI KWELI Video: Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah na Makamanda 24 walivyoshamabliwa hadi kifo

SI KWELI Video: Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah na Makamanda 24 walivyoshamabliwa hadi kifo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Hii hapa video ikionyeshanamna Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei na Makamanda wake 24 walivyoshambuliwa na Majeshi ya ushirika ya Israel na Mareani


Screenshot 2026-03-03 090223.png
 
Tunachokijua
Baada ya kifo cha Ayatollah Ali Khamnei Februari 28, 2026 baada ya mashambulizi yaliyofanywa na Marekani pamoja na Israeli.

Madai

Mtumiaji mmoja wa Instagram amechapisha video Machi 3, 2026 na kueleza kuwa ni ya shambulizi lililopelekea kifo cha Ayatollah Khamnei.

Uhalisia wa madai hayo ni upi?

Ufuatiliaji umebaini kuwa video hiyo haihusiani na tukio la kushambuliwa Ali Khamnei na kuepekea kifo chake Februari 28, 2026.

Kwa kutumia nyenzo za kidigitali ikiwemo google reverse image seaarch imedhihirisha kuwa video hiyo imekuwepo mtandaoni takribani miezi mitatu iliyopita. Mathalani Tazama hapa na hapa.

screenshot-2026-03-03-112015-png.3551541

Video hiyo ilisambazwa kuanzia Desemba, 2025 wakieleza kuwa Iran wameachia video hiyo kuonesha namna jeshi la Israeli lilivyashambulia jeshi lao wakati wa vita ya siku 12 iliyoanza June 13, 2025.

Ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa video hiyo imeunganishwa na video nyingine zilizotengenezwa kwa kutumia Teknolojia ya Akili Unde (AI)

screenshot-2026-03-03-101012-png.3551540
Back
Top Bottom