Video: Kocha wa Yanga na Wachezaji wa yanga walivyomfanyia fujo Mwamuzi baada ya mchezo

Stress mbaya sana, Embu angalia VIDEO ya Huyu Shabiki wa Utopolo mmojawapo ya Waliofanyafujo anavyobwabwaja ujinga.
aisee, hawa yanga wakikosa tena ubingwa msimu huu basi kazi ipo
 
Hivi lile kundi la simba ambalo limeandaliwa kuishambulia Yanga sijui mfadhili wake ni nani kila kukicha wako mitandaoni sijui hata kazi wanafanya saa ngapi yule mfadhili wa kikundi hiki atamaliza hela zake bure maana hatafanikiwa
 
Hivi lile kundi la simba ambalo limeandaliwa kuishambulia Yanga sijui mfadhili wake ni nani kila kukicha wako mitandaoni sijui hata kazi wanafanya saa ngapi yule mfadhili wa kikundi hiki atamaliza hela zake bure maana hatafanikiwa
Unateseka Kutokea pande zipi mkuu
 
Viongozi wa Yanga wachukue hatua mara moja ya kuwaonya wachezaji wao wasipambane au kubishana na marefa hata kidogo wala wasiwe wanasikiliza maneno ya kuwa refa huyu hatupendi au huwa anatuonea. Kwa mtu anayefahamu saikolojia ya mpira anajua wazi ukiweka kichwani kwako kuwa huyu muamuzi huwa anatuonea basi hata akifanya kosa la kibinadamu basi akili yote inaenda kuona kuwa ni uonevu. Na moja kwa moja mchezaji mmoja mmoja anaanza kujaa upepo na kutoka mchezoni halafu ikifika timu nzima imetoka mchezoni basi ndio dhahama inapoanzia hapo wachezaji kupata kadi na mwisho wa siku timu kupoteza mchezo na wachezaji muhimu kukosa michezo ijayo.

Suala la kubishana na marefa hilo waachiwe wapenzi na wanachama na katu isiwe kwa wachezaji kwani itaigharimu timu ya Yanga hasa kipindi hiki ligi inapoelekea mwishoni na kila mchezo sasa ni fainali. Namkumbuka mwalimu mmoja wa mpira alikuwa anafundisha timu za madaraja ya chini kwenye ligi ya mkoa zamani miaka ya themanini huko mchezaji wake akimlalamikia refa anatuonea yeye alikuwa anawahamasisha wachezaji wake wacheze mpira waachane na refa na wafuate kanuni zake mbili tu:
1. Pigeni mashuti makali nje ya 18 mfunge magoli halafu muone refa na mshika kibendera kama watasema ni off side
2. Pambaneni mfunge magoli ikiwezekana hata 100 refa hawezi kuyakataa yote, akikataa 50 atakubali 50.
Hiyo kanuni ya 1 ndio aliyoitumia Mukoko kwenye mechi na Kagera Sugar kusawazisha goli na ndio inayokubalika. Lakini kitendo alichofanya Kaseke kwa kweili kitamgharimu Kaseke mwenyewe na hata Yanga kwani kwa sasa yeye ni mchezaji muhimu sana akifungiwa wakati huu timu inapohitaji huduma yake itakuwa balaa sana. Chonde chonde viongozi wa Yanga narudia tena rudini kwa wachezaji wenu muwakataze wasicheze na marefa kazi yao iwe kucheza mpira tu kazi ya marefa wawaachie nyie mfuatilie kwa kufuata njia sahihi .

TFF na chama cha waamuzi nao wanapaswa waingilie kati kwani suala la marefa kufanya makosa sasa limezidi mpaka wakati mwingine mtu unajiuliza hivi kweli ni makosa ya kibinadamu au hao waamuzi wana lao jambo?
 
soka letu nΓ― tff na board ya ligi wanabingwa hao wamemuandaa
Utopolo mnaboa!! Mimi nawaunga mkono wekeni mpira kwapani mkimbilie ligi ya daraja la kwanza!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…