McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wakuu,
Nimekutana na video hii ya harusi ya watu wa kabila moja huko Nigeria, nimewaza sana kwa vyuma vilivyokaza sidhani kama wanaume wa Kitanzania hasa wa Daslam wangeweza.
Huu utaratibu uko huko kwenye kabila moja la Nigeria linaitwa Ijaw ambapo mwanamke akiwa Bi Harusi kwenye harusi yake hatakiwi kucheka mpaka aridhishwe na kiwango cha pesa au zawadi ambazo mmewe amempa.
Yaani mwanaume hapo unatakiwa utoe zawadi hadi pale mwanamke wako atakapofurahi na kuridhika. Akiona hela ulizogawa ni ndogo au hazijamridhisha basi hatocheka na unatakiwa utoe hadi atakapocheka.
Sasa nimewaza kwa hawa wanawake zetu wa Kitanzania ambao baadhi yao ni kausha damu akina Mwajuma Ndalandefu kwa utaratibu huu si unafilisika?
Yaani nimewaza wakina Zaituni, Mwanaenzi na kina Farida wanaokaaa kule Uswahilini ndo wanapata fursa ya kuwa kama huyo dada hapo, hivi kibongo tungeoa kweli wakuu?