Video: Lori la mafuta lapata ajali Songwe. Wananchi hawajifunzi, wahangaika kujichotea mafuta ya bure

Video: Lori la mafuta lapata ajali Songwe. Wananchi hawajifunzi, wahangaika kujichotea mafuta ya bure

Wakuu,

Kwenye hii video huyu ni dereva wa hili lori akirekodi tukio zima kwa ajili ya kumuonesha bosi wake.

Ni hasara.

Kilichonisikitisha zaidi ni kuona kuna watu wanachota mafuta hapo wakisahau kabisa kuwa hilo gari likilipuka ni hatari sana kwao.

Watu wana confidence sana kwa kweli. Mimi nikiwa kwenye daladala au private car nikipishana tu na lori la mafuta napata trauma ila watu wana ujasiri kabisa na kwenda na madumu ya mafuta kukinga.

Nimepata maswali mengi mno.

View attachment 3182680
Uhai hauna thamani mbele ya mali!
 
Hayo maeneo kawaida, tena ikitokea umepata ajali y’a bus wakija kung’ang’ania pochi yako au simu we waachie lasivyo wanakuzima.!!
Watu wa maeneo hayo ni makatili usiombe ukutane nayo.!!
 
Kuna siku tumetoka morogoro na bus katikati hapa tukakuta gari la mafuta limepigwa ubavu na gari nyingine kubwa mafuta yanadondoka lami yamechora mbali kweli wakati tunapishana na hiyo gari moyo unadunda najua iliyomwagika petroli hata cheche tu inaweza ikatukaanga ndani ya gari tukafia wote humo kwa kukosa hewa ama kukanyagana kwa hofu moto ukiwaka kulizunguka gari.
Najiuliza bado watu hawajui thamani ya uhai ni zaidi ya hayo mafuta ?
 
Hii inaashiria kuwa wtz ni masikini wa kutupwa..mama Samia kavuruga uchumi wetu ndiyo maana wtz wamekuwa wanagombania mafuta
 
Moto ukiunguza kende na Kei zao ndio utakuwa mshahara wako halali.

Wangese sana hao watu pori.
 
Watu hawana cha kupoteza, ni kama vile mtu anasema hunijui sikujui Mimi nikifa sikuongezei Wala kukupunguzia chochote.
 
Haya yote yanasababishwa na ukosefu wa elimu
 
UMASKINI WA KUPITA KIAS ..ASILIMIA.KUBWA YA WATANZANIA NI MASIKINI
HAKUNA SABABU NYINGINE.
KATAA UMASIKINI.
 
Watu washajitoa mhanga, ni vigumu kuacha fursa kwa usawa huu, tatizo hapo ni umasikini
 
Back
Top Bottom