nina uhakika Hamas hawakutarajia hiki kilichotokea, kama wangekuwa wametarajia wasingeanzisha hii vita. naona hata hezbollah wanaingiza mguu na kutoa manake wanajua sasaivi majengo yetu yatakuwa vumbi kama gaza. hezbollah walipiga mkwara kwamba israel ikiingia tu gaza wao wataingia vitani, ila wamepoa sana. hamas walijua wakianzisha vita na kwasababu wanayo mateka, basi vita itapigwa kwa wiki kadhaa, israel itaua wengi na dunia itapiga kelele dhidi ya israel na israel itasitisha mapigano aidha kwa kubadilishana mateka au kwa kelele za mataifa mengine.
sasa israel akatoa amri raia watoke kaskazini, wametoka karibia wote na waliobaki wamesema kuanzia kesho kutakua na cease fire ya masaa manne kila siku kuruhusu raia kuondoka, pale watabaki hamas peke yake (kule kaskazini) na wakibaki, hakutakuwa na sababu ya cease fire tena, iran hatakua na uwezo kuwapa siala, watatumia silaha zote, watatumia chakula chote, maji yalishakatwa, umeme hakuna, majenereta kupeleka hewa kwenye mahandaki yatakuwa hamna mafuta, hivyo hamas watajisalimisha na watafutwa kabisa. walipiga mahesabu vibaya sana.
hapo sasa, hata zile hospitali za Gaza hazitakuwa salama tena kwasababu watu wanaotakiwa kutibiwa wameenda kusini, wafanyakazi watatakiwa kuondoka, UN pia watatakiwa kuondoka kwasababu pale raia hawapo napameshakuwa eneo la vita.