DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Hali ya mvutano imetokea baina ya mawakili wa Jamhuri na baadhi ya mawakili wa upande wa Tundu Lissu, pamoja na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakigombea sehemu ya kukaa ndani ya ukumbi wa Mahakama Kuu, Masjala ndogo ya Dar es Salaam.
Mvutano huo ulijitokeza baada ya Jaji kutoa mapumziko ya dakika 30, ambapo pande hizo zilianza kutupiana maneno kufuatia kutokuelewana kuhusu mpangilio wa viti ndani ya ukumbi huo.
Tofauti na siku nyingine ambazo kesi hiyo imekuwa ikiendelea, leo idadi ya wafuasi na wafuatiliaji ilikuwa ndogo, wengi wakiwa ni mawakili wa pande zote mbili na baadhi ya maofisa wa Mahakama. Wanachama na viongozi wa CHADEMA waliokuwa wakifuatilia kesi hiyo walionekana kuwa wachache zaidi kuliko siku za nyuma.