Pre GE2025 Video: Mbele ya Rais Samia, Mbunge wa HandenI atangaza kuoga hadharani pindi mradi wa maji wa jimboni kwake utakapomalizika!

Pre GE2025 Video: Mbele ya Rais Samia, Mbunge wa HandenI atangaza kuoga hadharani pindi mradi wa maji wa jimboni kwake utakapomalizika!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Harakati za ku-please wananchi katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye kampeni zinaendelea.

Mbunge ambaye alikuwa ana miaka 5 ya kuwaletea maji wananchi leo hii anasimama mbele ya Rais anasema kabisa kuwa siku maji yakija ataoga hadharani.

Mbunge wa Handeni akiwa anaongea mbele ya Rais Samia ambaye yuko kwenye ziara ya kikazi mkoani Tanga alisema:

"Mheshimiwa Rais kwa furaha niliyonayo mimi Mbunge wa Handeni, siku maji yatakapotiririka baada ya mradi huu mkubwa kukamilika mimi nimewaahidi wananchi hawa nitaoga hadharani. Hicho mnachosubiri kukiona hamtakiona maana ntaoga na nguo"


 
Back
Top Bottom