Mimi nawaza sana hivi huyu Rais m-CCM kuliko wote jamani wana JF, akishinda safari hii ya mwisho wake, nawaza tu mtakavyo koma, watanzania yaani nawahurumia, safari hii ni kata funua balaa bin mikosi, hatumii risasi wala watekaji tena, si anajua hawaitaji tena na hatashtakiwa sasa je!
km aliwaburuza kwa style ile ya dharau wakati anajua umuhimu wenu kwenye box la kura! sasa hii ni safari ya mwisho lala salama haitaji kura zenu tena ! mwinyi, Kikwete walijibembeleza kura pale Lumumba. huyu mwenzangu na mimi bado anakejeli wapiga kura! anakamata na kuwabana wapinzani waziwazi tena kipindi hiki!
Msimpe kura ikitokea kapita huyu bwana muanze kulia mapemaa na wake zenu na kumkingia makalio mvae bukta nzito 2, ili awachape viboko panapostrahili! mkikaa vibaya viboko vita ingia machoni kwa hasira zake mtakosa kuona milele!
Jiwe anani kumbusha Indunas wapya Nyakato Secondary school -Bukoba jamani Khaa! Lawi ndege huyu jamaa sijui yuko wapi!!
Wanaojifanya kujigaragaza chini atawageuka kinyonga akasome!!! ataanza nao hao! haaminiki huyu! jiulize Lugola yuko wapi, Nape, January makamba? hawa walicheza michezo hatari kwa ajili yake akamate madaraka!!!
Bashite ana nafasi yake hapo imetulia. nilijuta sana kumpa kura yangu!