Nadhani huenda kuna maelezo na mambo mengine mengi ambayo hayajawekwa wazi. Mil 150 tena ya mkopo halafu marehemu akafariki kabla hajamaliza haiwezi kufanya wachukuwe hatua za kishenzi namna hii (hii nawaza mimi tu lakini Bongo inawezekana). Halafu namna wanavyombeba... kuna kitu hatujui kwa undani.inasikitisha sana
Niliona matangazo ya maeneo ya Mikocheni few months ago
Mikocheni 380sqm vile viwanja vimefatana eneo moja ni 375m sasa ikiwa na nyumba nzuri bombaa lazima zaidi. hicho kinaonekana ni kikubwa hivyo lazima watu wapige dili walioona mjane atashinda.
Ukiona pamefika hapo maana yake makubaliano yashashindikana kitambo sanaThamani na nyumba na Kiwanja hapo Mikocheni, mbona ni mara Tano ama Sita ya hicho kiasi anachodai
Wakubaliane, mjane apewe muda zaidi aweze kutafuta hicho kiasi
Auze hiyo nyumba Kwa milioni 800 ama 950 then alipe hilo deni kisha akanunue Kiwanja Kigamboni ajenge nyumba nyingine ya milioni 400 hivi, huku kiasi kingine atumie kufanya biashara
Hakuna taharuki yeyote..Taharuki kubwa imeibuka Mikocheni jijini Dar es Salaam, baada ya mjane Alice Haule kuvamiwa na watu kwenye nyumba yake aliyoachiwa na marehemu mumewe, Justice Rugaibula kisha kumtoa kwa nguvu pamoja na wapangaji wenye asili ya Kichina, waliokuwa wakiishi kwenye nyumba hiyo.
Taarifa za awali zinadai kuwa marehemu mumewe, alikopa fedha kutoka kwa mfanyabiashara mmoja, kiasi kinachotajwa kuwa ni shilingi milioni 150, ambapo alianza kurejesha lakini kabla hajamaliza, akafikwa na umauti.
Mvutano huo ukapelekwa mahakamani ambapo inadaiwa kuwa kabla ya muafaka kufikiwa, ndipo walipokuja kutolewa kwenye nyumba yao.
Video: Global TV
Ajabu, hata si bei ya kiwanja.Hii awamu matapeli na madhulumati yamefufuka, yaani mikocheni hii nyumba tena ya ghorofa moja iwe na thamani ya milioni 100 huyo mama ametapeliwa mchana kweupe
Mbona kama naona jinai hapa!? Hasa uhusiano wa kuanza kurejesha na umauti? System kama haipo paralyzed Kuna kazi ya kufanya hapa!....kiasi kinachotajwa kuwa ni shilingi milioni 150, ambapo alianza kurejesha lakini kabla hajamaliza, akafikwa na umauti.....
Inawezekana sahihi usemacho, ila vyema akashauriwa afanye hivyoUkiona pamefika hapo maana yake makubaliano yashashindikana kitambo sana
DuhHuyu mama anayebebwa kama kiroba nadhani ni dada yake kabisa wa mama na baba mmoja na Profesa J. Sema mwamba naye sijui bado anapambania afya yake vinginevyo labda angekuwa keshaingilia kati.
Mama kasema nyumba yake ina thamani ya bilioni mbili na akitaka kuiuza hata leo kwa kiasi hicho anapata. Leo wajanja wanataka kumtoa kwa nguvu kwa deni la milioni 150 kisa wana barua ya mkuu wa Wilaya. Mkuu wa Wilaya tangu lini ndo amekuwa mahakama? Nchi ya ajabu sana hii!
Mange ameandika undani wake. Hii ni kazi ya mafisadi walio chini ya Abdul. Wanataka kiwanja wajenge apartments. Amri zinatoka moja kwa moja ''kutoka juu''. Kila mtu anaogopa kumsaidia mjane wa watu kwa sababu kuna mkono kutoka juu unaelekeza kila kitu.View attachment 3478169
JE KUNA ANAYEJUA CHOCHOTE KUHUSU HUYU MJANE ANAYE DHURUMIWA MAKAZI YAKE HAPO DSM...MAANA INA SIKITISHA NA KUUZUNISHA SANA
PUBLIC NEED CLARIFICATION
UMMA TUNAHITAJI TUJUE KINACHO SABABISHA HII SHIDA....
Mh,hatariHao jamaa wameona nyumba ina dhamani kubwa kuliko mkopo wanaoudai wanataka kutumia dhuluma