VIDEO: Mjane wa Justice Rugaibula avamiwa, atolewa kwenye nyumba aliyoachiwa na mumewe pamoja na wapangaji wengine

inasikitisha sana

Niliona matangazo ya maeneo ya Mikocheni few months ago
Mikocheni 380sqm vile viwanja vimefatana eneo moja ni 375m sasa ikiwa na nyumba nzuri bombaa lazima zaidi. hicho kinaonekana ni kikubwa hivyo lazima watu wapige dili walioona mjane atashinda.
 
Nadhani huenda kuna maelezo na mambo mengine mengi ambayo hayajawekwa wazi. Mil 150 tena ya mkopo halafu marehemu akafariki kabla hajamaliza haiwezi kufanya wachukuwe hatua za kishenzi namna hii (hii nawaza mimi tu lakini Bongo inawezekana). Halafu namna wanavyombeba... kuna kitu hatujui kwa undani.
 
kama babu zetu walikuwa wanauzana wenyewe kwa mzungu Basi haishindikani huyo mama kutapeliwa kanyumba kake kwa hao wachina tena nguvu kama hiyo.


Watu wanachakarika kutoa vitu nje, hawajiulizi mara mbili mbili
 
Ukiona pamefika hapo maana yake makubaliano yashashindikana kitambo sana
 
Hakuna taharuki yeyote..
Dingi hakuwaambia kila kitu
 
Hii awamu matapeli na madhulumati yamefufuka, yaani mikocheni hii nyumba tena ya ghorofa moja iwe na thamani ya milioni 100 huyo mama ametapeliwa mchana kweupe
Ajabu, hata si bei ya kiwanja.

Serekale iko mifukoni kwa watu.
 
Uku kwetu Malawi Kuna wafanya biashara walikua na kawaida ya kukopesha wafanyabiashara wengine pesa dhamana ikiwa ni nyumba au kiwanja (zilizo Prime Areas)
Utakapo Fanya marejesho wanakugeuzia kibao either kwa kuweka riba kubwa zaidi au kukataa pesa zako mpaka ule muda ulio kua mmekubaliana deni liwe lime isha una fika hivo Wana tumia mabavu kuchukua nyumba/kiwanja kwa kua huja walipa kwa wakati.
Wakati mwengine walikua na uwezo hata wa kuchukua uhai wako Kisha Wana kuja kudai madeni wakiwa na vithibitisho hivyo mlio Baki mkishindwa kumlipa wanachukua dhamana zilizo wekwa (nyumba/kiwanja)
...
Ni siku nyingi sasa zime pita sijui kama bado Wana endelezwa hiyo michezo au laa maana sipo Tena uko

Khan Yunis,
Palestine.
 
Ukiona pamefika hapo maana yake makubaliano yashashindikana kitambo sana
Inawezekana sahihi usemacho, ila vyema akashauriwa afanye hivyo

Akiendelea kukaidi, anaweza hata kupotezwa

Maana kwasasa Nchini, unaweza kutekwa na gangsters ama wasiojulikana
 
Huyu mama anayebebwa kama kiroba nadhani ni dada yake kabisa wa mama na baba mmoja na Profesa J. Sema mwamba naye sijui bado anapambania afya yake vinginevyo labda angekuwa keshaingilia kati.

Mama kasema nyumba yake ina thamani ya bilioni mbili na akitaka kuiuza hata leo kwa kiasi hicho anapata. Leo wajanja wanataka kumtoa kwa nguvu kwa deni la milioni 150 kisa wana barua ya mkuu wa Wilaya. Mkuu wa Wilaya tangu lini ndo amekuwa mahakama? Nchi ya ajabu sana hii!
 
Case solved hii! Namuona Mh Chalamila keshafika mapema sana! Tengeneza tatiozo tatua tatizo
 
Duh
 
Your browser is not able to display this video.



JE KUNA ANAYEJUA CHOCHOTE KUHUSU HUYU MJANE ANAYE DHURUMIWA MAKAZI YAKE HAPO DSM...MAANA INA SIKITISHA NA KUUZUNISHA SANA

PUBLIC NEED CLARIFICATION


UMMA TUNAHITAJI TUJUE KINACHO SABABISHA HII SHIDA....
 
View attachment 3478169


JE KUNA ANAYEJUA CHOCHOTE KUHUSU HUYU MJANE ANAYE DHURUMIWA MAKAZI YAKE HAPO DSM...MAANA INA SIKITISHA NA KUUZUNISHA SANA

PUBLIC NEED CLARIFICATION


UMMA TUNAHITAJI TUJUE KINACHO SABABISHA HII SHIDA....
Mange ameandika undani wake. Hii ni kazi ya mafisadi walio chini ya Abdul. Wanataka kiwanja wajenge apartments. Amri zinatoka moja kwa moja ''kutoka juu''. Kila mtu anaogopa kumsaidia mjane wa watu kwa sababu kuna mkono kutoka juu unaelekeza kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…