Video: Mjomba wa Bibi harusi apokea kipigo kizito akidaiwa kumsifia Rais Samia kwenye harusi

Wakuu

Nimekutana na hii Video inayosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii inamuonesha mjomba wa bibi harusi akipokea kipigo baada ya kudaiwa kumsifia Rais Samia kwa kusema "Samia ni rais mzuri"

Imetengenezwa hii, ili kufurahisha na kupotosha watu. Ni dalili za kushindwa, katika mapambano ya hoja, na sasa mmekimbilia katika propaganda. Mtawapata wajinga tu.
 
Thanks God,ila natamani mjombq angekuwa baba levo,au zile chawa zingine,walahi ningesherekea kama nimepata Jimbo jipya
 
Dah watu wa humu hasa anti government hawana reasoning kabisa. Wakisikia ishu ya ovyo ihusuyo Maza ghafla wanakomenti kwa kuunga mkono . Ajabu ni kwamba wote hujifanya ni wenye fikra pevu kuliko yeyote! Huyu apigwaaye hapo anaonekana kabisa ni aina ya mtu aliyevamia sherehe hiyo either kwa kuiba au kwa namna flani ya vurugu dhidi Yao. Hili moja. Mbili niliwaambia kuhusu Habili kwamba ni mtu anayewachezea akili zenu! Vitu anavyoongea ni general hata ninyi wote mnavijua! Hana hoja zaidi ya uwongouwongo. Ajabu ni kwamba majibu ya wapingaji ikawa ni matusi kwamba nalipwa posho ya kumtetea Maza.
Juzi namba 1 amezushiwa kadedi . Aliyeanzisha ni walewale wazushi. Kuweni na reasoning. Anyway chuki zipo kweli dhidi ya hali hii lakini muda flani lazima tuhoji hiki kimetoka wapi! Kina ukweli gani? Hii itasaidia kufanya hata wageni wanaotembelea humu Kuona yes jukwaa hili ni jukwaa la wataalam na wazoefu .
 
Mbona mjomba mwenyewe upinde? Inaonekana

Halafu hii thread ilitakiwa iende jukwaa la chit chat kule huku ni kulidhalilisha jukwaa la siasa

Hizi ni shughuli za uswahilini hazihusiani na hayo masuala uliyoleta wewe
Leta mada ni pumbavu kama mipumbavu mingine
 
Dah watu wa humu hasa anti government hawana reasoning kabisa. Wakisikia ishu ya ovyo ihusuyo Maza ghafla wanakomenti kwa kuunga mkono . Ajabu ni kwamba wote hujifanya ni wenye fikra pevu kuliko yeyote! Huyu apigwaaye hapo anaonekana kabisa ni aina ya mtu aliyevamia sherehe hiyo either kwa kuiba au kwa namna flani ya vurugu dhidi Yao. Hili moja. Mbili niliwaambia kuhusu Habili kwamba ni mtu anayewachezea akili zenu! Vitu anavyoongea ni general hata ninyi wote mnavijua! Hana hoja zaidi ya uwongouwongo. Ajabu ni kwamba majibu ya wapingaji ikawa ni matusi kwamba nalipwa posho ya kumtetea Maza.
Juzi namba 1 amezushiwa kadedi . Aliyeanzisha ni walewale wazushi. Kuweni na reasoning. Anyway chuki zipo kweli dhidi ya hali hii lakini muda flani lazima tuhoji hiki kimetoka wapi! Kina ukweli gani? Hii itasaidia kufanya hata wageni wanaotembelea humu Kuona yes jukwaa hili ni jukwaa la wataalam na wazoefu .
UMEMALIZA KABISA, SIONGEZI NENO. Inasikitisha lakini kuona kuwa ukweli huu ulioandika unaweza ukaambulia matusi kadhaa kutoka kwao 'think tanks' wa gen z waliopo humu. Ukweli ni kuwa wanakurupuka nmooooo.
 
Ila Wabongo kwa uzishi hawana mfano. Walevi wana ugomvi wao wanasingizia kisa kasifia rais!

Sawa na uzushi wa Davido kusapoti maandamano TZ wakati wa show yake in reality alikuwa shabiki mwenye bendera ya TZ ndani ya ukumbi and the camera happened kumuonyesha. Wabongo wakapita nayo.
 
Back
Top Bottom