VIDEO: Mke wa Balozi amuanika mumewe

VIDEO: Mke wa Balozi amuanika mumewe

Wanawake wanasingiziwa mengi jamani. yaani mtu anatakiwa avumilie tuuuu maovu ya mume
masuala ya ndoa si ya kuingilia na kumhukumu mmoja pasipo kumsikiliza mwingine. Ukimsikiliza mwenzake si ajabu ukakuta mlalamishi ndiye tatizo kubwa. Mwanaume hawezi akafikia kufanya hivyo pasipo sababu, hasa kutendwa.
 
Ubaya wa wanandoa.. Utatoka povu na kuchukua upande wa mtu ila kesho wanarudiana alafu wewe ndio unageuka bad guy kwenye story..
Cha kufanya ni kusubiri wote waongee, pima uzito, washauri unaloona linafaa af pita kushoto kama hakijatokea kitu
 
Ukweli ni kwamba ndoa ni taasisi isiyostawi kwa mabadiriko maana ina misingi ya asili kwamba mke atakuwa chini ya mme na atatawaliwa naye akiwa mnyenyekevu, heshima na msikivu.
Mme atabak na jukum moja la kumpenda mkewe!
Asiyekubaliana na hili asijiingize kwenye taasisi hii, atamaliza vibaya na kuwasumbua watu.(You can't eat your cake and have it)
WE LIVE ONCE, LIVE RESPONSIBLY!
 
Wanawake wanasingiziwa mengi jamani. yaani mtu anatakiwa avumilie tuuuu maovu ya mume
Sasa yeye si ndie kaanzisha. Siku zote anaemaliza ugomvi ndio anaonekana mkorofi. Yaani mwanaume aanze tu kuwehuka bila sababu.

Zamani mwanaume akizinguana na mkewe jamii nzima tunakuwa team m'moja na mke wa jamaa tunamtetea bila kuhoji yaliyotokea awali ya yote. Ila miaka hii imeshaonekana wazi kuwa wanawake ndio wakorofi na visa vyao huanza mapema sana.

Mwanamke anaweza kupika chakula vibaya makusudi na ukimhoji anakuja juu kuwa si ni bahati mbaya umsamehe na bado akaka siku mbili akarudia tena, hapo bado uzembe kwenye usafi wa nyumba na watoto, na matumizi mabaya ya pesa za familia. Mwanaume stress zikikushika unatamani kumtandika makofi unaona hapana nisipate lawama za bure, unaamua kutafuta mwanamke mwingine maisha yaendelee. Utashangaa sasa mkeo kiburi anaanza kukujazia watu na kulalamika kuwa naonewa kijinsia na upuuzi mwingine.

Siku hizi jamii imeshawajua so mwanamke kama huyu anayelalamika kwanza kwa kumtazama tu the way anaongea unajiridhisha kuwa mwanaume alikuwa anavumilia mengi sana hadi kufikia hatua ya kumtoroka.
 
TAA NDOAA... sasa mwanamke kama huyuu mdomoo mrefu hivii maneno kibao ukisema umuoee si kutaka kufa kabla ya siku zako

Naona umepata sababu za kuhalalisha kula kimasikhara 😁😁
By the way kama ndoa unaitaka, tafuta mwenye madhaifu unayoweza kuyavumilia ila kutumaini mtu atabadilika ni sawa na kuziba jua kwa ungo
 
Wanawake wanasingiziwa mengi jamani. yaani mtu anatakiwa avumilie tuuuu maovu ya mume
Zipo taratibu za watu waliostaarabika kutatua migogoro yao japo ni kweli hatujui full story ila swala la kuanikq mambo ya ndani ni swala la kipumbavu sana
 
masuala ya ndoa si ya kuingilia na kumhukumu mmoja pasipo kumsikiliza mwingine. Ukimsikiliza mwenzake si ajabu ukakuta mlalamishi ndiye tatizo kubwa. Mwanaume hawezi akafikia kufanya hivyo pasipo sababu, hasa kutendwa.
Unaonaje swala la kuanikq video ya namna hii?
 
Ubaya wa wanandoa.. Utatoka povu na kuchukua upande wa mtu ila kesho wanarudiana alafu wewe ndio unageuka bad guy kwenye story..
Cha kufanya ni kusubiri wote waongee, pima uzito, washauri unaloona linafaa af pita kushoto kama hakijatokea kitu
Mkuu swala langu ni mwanamke kuanika mitandaoni mambo y ndoa yake

Halikubaliki zipo taratibu za kusolve issues zao lakini sio hivi

Hayo mengine hayanihusu
 
Back
Top Bottom