VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

VIDEO: Msanii Roma na wenzake warejea rasmi uraiani. Kufunguka Jumatatu

Mods tafadhalini tupeni tu thread moja ya kumuhusu Roma Mkatoliki kwani naona sasa kila Mtu ' anaibuka ' tu na ' angle ' ile ile inayofanana na za wengine na ' kukurupuka ' kuileta humu hadi sasa inaboa. Kama vipi na hii nayo itupieni kule na msichoke kuziunganisha tafadhalini.
Ili nalo neno.
 
Kwani kinachomfanya ashindwe kuongea yaliyomsibu leo (jumapili) ni nini mpaka tusubiri juma3. Kuna jambo zito nyuma ya pazia, na si bure. My take, Juma3 itafika na sinema itaendelea. Sasa hivi ni mwendo wa matukio aka headlines alimradi 2shindwe kujadili kwa kina mustakabali wa maendeleo ye2 kama Taifa.
 
Inaelekea pesa ndefu wamevuta hata Mimi nisingeongea... Hapo ndipo wanamshusha Nape ati raisi aunde tume?

Hawa wapumbavu wanacheza ngoma ya msubi nasi ndio tuna fuata midundo ya ngoma yenyewe... Akili ndogo kuongiza akili kubwa...
 
Wote mnaotaja jina la Mungu kwa kumuonea huruma huyu kijana ni wanafiki,wazandiki,pumbavu zenu,(sio tusi) huyu kijana katumika na Bashite, wote mnajua police wakiokoa watu waliotekwa ambavyo inavyokuwa, Siro angekuwa amefanya press mara elfu kumi
 
Hii inshu imejawa na Usaniii tu kwa vision yangu Mawili either Wametaka mzee wa Mtama leo asitokee kwa Front Pages za Magazeti
 
Vijana wa idara ya Usalama wana akili kubwa, hasa wale waliokosa ajira kwenye mchujo wa Interview CIA, MUSSAD, TISS (Tanzania), n.k.

Kuna watu wanaishi kwa kusumbua na kuhangaisha industries na brand za watu. Wengi wao huwa ni wanasiasa hasa pale wanapotaka kuwa na status kama za wananchi wao...meaning, kiongozi anaweza kuwa hata ni fukara asiye na elimu, lakini ana kipaji cha uongozi, anaowaongoza wengine ni matajiri kumzidi, so tatizo huja pale anapotaka kuwa tajiri kama wao...HII NDIO SABABU HAKUNA MWANASIASA TAJIRI AMEWAHI KUWA LISTED KWENYE FORBES, AU ORODHA YA MATAJIRI DUNIANI.

Professa J, Babu Tale, Roma na uongozi wako, Diamond Plutnumz, RC Makonda, Nape na Baraza la Waandishi wa Habari Tanzania; acheni kusumbua watu, tuacheni tufanye kazi.

Mnachokifanya sio kipya, kila Ikulu, kila ofisi ya Mkoa katika kila nchi hizo ndio shughuli zake. Kinachonishangaza iweje watu wazima kama nyinyi mnaojinadi wazalendo ndio muwe wa kwanza kununuliwa?? What is money to you guys? Coz kama ni hela mnayo, shida ni nini, majina?? Mbona mkuu wa mkoa kachafua majina ya watu lakini ndo kwaaaanza wanapiga kazi?

Anyway, ila kwa sasa, kitengo cha TISS kina sifa mbaya kimataifa ya kukosa weledi na kuheshimu taaluma ya usalama na kinalijua hilo. Mfano hai ni Wapelelezi 19 kukamatwa Malawi.....19 🙂 🙂 🙂 🙂 🙂

Niweke bayana kuwa Dar es Salaam ndio Tanzania, na mikoani ndio kuna Wakuu wa mikoa...Mkuu wa mkoa Dar es Salaam (capital city) ni mlinzi wa mali za Rais wa nchi. Hivi ndivyo ilivyo hata Ulaya.

Tatizo RC wa sasa ni limbukeni wa mafanikio na utajiri. Naomba mjifunze kwa kinachomtokea Zuma kule South Africa sasahivi...kama kuna Rais ambae kawekwa kitimoto na amekalia ncha ya mkuki ni Jacob Zuma...kwahiyo kwa Magufuli tutasubiri sana...

Tekeni, teseni, uweni, yayusheni maiti kwa kemikali...hakuna mwenye muda na nyinyi, maana mnafanya kazi yenu, na mnajulikana na mnashiriki shughuli za kijamii kama vile kutuma hela kwa M_pesa, michango ya harusi na ibada za maombezi...lakini mkiona tumeanza kuwaua nyie, tumewavamia pale Masaki, tumeiteka TBC...mjue kuwa mlivuka kiwango na kuamsha hasira zetu.

Bunduki kitu gani bwana...kila mtu akiamua anaweza kuimiliki. Wakurugenzi wa makampuni Dar wanalijua hili.

Yaani Magufuli tukimwita Dikteta mie naona tunampa sifa za bure tu...huyu hana huo ubavu, sio kwa Tanzania hii, sio kwa Tanzania ya Nyerere aisee...hii Nchi inalindwa!!! tena kwa satellite za USA, Urusi na ulimwengu usioonekana...ACHENI UJINGA.

Hakuna mpumbavu anayeweza kuiyumbisha Tanzania to a National Scale, kwaito zao zitaishia kwenye Media na kwa watu binafsi walio na maslahi yao. Mfano ni Media kukataa kumpromote Bashite lakini leo hii kawazidi akili, pia njaa imewalemea, imebidi wao ndio wamfuate.

Kwa sasa kila mtu anapigania tumbo lake tu...sio Diamond, Tale, Majizzo au Harmo Rapa. POLITICAL ACTIVIST WA KITANZANIA KWASASA NI WAWILI TU: Mange Kimambi na Ben Saanane aliyepotea...siku ukipotea utajua kwanini.

Mange anaripoti kituo cha polisi kila siku pale USA kwaajili yetu watanzania...Hakuna mapinduzi ya Nchi yaliyoletwa huku ukiwa unaishi hapo hapo nchini! ukibisha kamuulize Kagame, Museveni na wengineo. Ndio maan Ben kapotea...it"s that simple.

Roma, kwani ungeniomba hiyo Milioni 14 hata mimi kuepuka usumbufu uliowasababishia WatanzaBia nisingekupa? umejua wananchi tumeingia hasara kiasi gani kwa faida zako binafsi ili hali unajua wewe sio wewe tena bali ni kioo cha jamii/brand? Kwanini umechangia kuongeza chuki kwa RC wa Dar es salaam?? (ninaposema RC ninazungumzia kiti, sio mtu a.k.a. Paul Makonda....kwasasa nikija Dar huwa naiona haina aliyeketi hapo na kuna umuhimu wa hio zabuni kutangazwa).

[HASHTAG]#ImOut[/HASHTAG]
M14
 
Haswa ndiyo ilikuwa nia yao.
Sasa Raisi ni Muhimu sana Kumwajibisha Muwakilishi RC kwa haya yanayoendelea Tz inaelekea pabaya sana
Dar hio ndio mji Mashuri na engine ya Tanzania sasa kama Inaendeshwa na Huyo jamaa huoni ni Kuirudisha nyuma mana watendaji wote kuanzia Kina Sirro,OCd wanasikiliza Older tu kutoka kwa jamaa, Very sad
 
Aliyetekwa alikuwa Dr ulimboka.nyie MNA cheza na akili zetu
Njaa ni kitu kibaya sana boss sasa sijui Roma kapewa ngapi? Master mind wa Hio Mission amefeli sana na soon wakina Roma wataonekana kama toilet Paper tu, Worthless kabisa
 
Njaa ni kitu kibaya sana boss sasa sijui Roma kapewa ngapi? Master mind wa Hio Mission amefeli sana na soon wakina Roma wataonekana kama toilet Paper tu, Worthless kabisa
Wapuuzi sana.MTU anasema watapatikana kabla ya jumapili na kweli wamepatikana.utasema wametekwa hawa?
 
Wapuuzi sana.MTU anasema watapatikana kabla ya jumapili na kweli wamepatikana.utasema wametekwa hawa?
Ni Drama kukipoteza kwenye Media Mkutano Wa Nape Huko mtama, Leo Front page ni Roma tu mkuu, Bashite apo anaona amecheza vizuri karata yake, Ila itakula kwake huyo aliekubali Atumike kama kondomu
 
Mhhhhhhhhhhhhh. Hayo makubaliano ya kuachiwa kama yanawabana sasa wasiongee kitu, ninashindwa kujua jumatatu kama wataongea kwa uhuru au wataongea kwa mujibu wa hayo makubaliano ya kuachiwa.

Tanzania my mamaland!. Tunatabasamu nyuso mioyo ikivuja damu. Nadhani amesahau kuishukuru serikali kati ya wale aliowashukuuru kwa kuwapigania.

Ninatamani na Saanane aachiwe kwa makubaliano ya kuachiwa.
Muda ni mwalimu nguri, atatoboa siri zote. Tusubiri tu japo yaweza isiwe j3
 
Back
Top Bottom