Nakuwekea kwa kiswahili
Katika gazeti la kimataifa la, Newsweek October 31, 1988, p. 44., lililobeba makala yenye kichwa 'Oo Bwana, Nani Aliyeandika Dua hii?'
kikosi cha wanatiolojia kutoka katika dhehebu kuu la kiporestanti, pamoja na Wasomi muhimu wa Biblia wa Kikatoliki nchini Marekani, baada ya ukaguzi wa kina wa miswada ya mwanzo kabisa ya Agano Jipya, wamehitimisha kuwa maneno pekee ya "Dua ya Bwana" Luka 11:2 na Mathayo 6:9-10. ambayo yanaweza kunasibishwa barabara na Yesu Kristo ni "baba".
Na hilo, ni kwa mujibu wa wasomi hao wa kanisa, maneno yote yaliyokuja baada ya ibara ya kwanza, "Baba yetu", ambayo ni dua muhimu sana ya Kikristo, yaliongezwa karne nyingi na waandishi wa kanisa walionukuu miswada ya mwanzoni ya Injili.
Shirika la U.S News & World Report, linanukuu zaidi kuwa, kikundi cha wasomi kilisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maneno yaliyoandikwa katika Injili kumhusu Yesu huenda ni ya kubuniwa.
Miongoni mwa hayo likiwemo neno la Ekaristi ya Yesu katika Karamu ya Mwisho ("Chukua, kula. Huu ni mwili wangu…") na kila neno aliloambiwa kuwa amelitamka toka msalabani.
Dr. J.K. Elliott, wa kitengo cha Thiolojia na Tafiti za Kidini wa Chuo Kikuu cha Leeds, ameandika makala iliyochapishwa katika jarida la The Times, London (10 Septemba, 1987) yenye kichwa "Kutazama mizizi ya Biblia".
Ndani ya makala yake, ameeleza kuwa: "Zaidi ya miswada 5,000 inayojumuisha Agano Jipya lote au sehemu yake iliyo katika lugha ya asili.
Miswada hii imepangika katika madaraja ya kuanzia karne ya pili hadi kuvumbuliwa kwa uchapaji. Imekisiwa kuwa hakuna hata watu wawili wanaoafikiana kwa kila kitu.
Bila shaka, maandishi yote ya mkono yanastahili kuwa na makosa ya bahati mbaya wakati wa kunukuu. Hata hivyo, katika kazi za kitiolojia si jambo la kushangaza kuwa mabadiliko ya kufikirika sana yaliingizwa ili kuondosha au kubadili maelezo ambayo waandishi wanayaona kuwa hayapendezi. Pia kulikuwa na mwelekeo wa wanukuzi wa kuongeza ufafanuzi au fasiri.
Mabadiliko ya hadhari yanadhaniwa kuwa yameingizwa katika zama za mwanzo kabla ya kuanzishwa hali ya kanisa ya Agano Jipya.
Mwandishi aliendelea kufafanua kuwa "hakuna hata mswada mmoja wenye matini isiyobadilishwa kutoka katika uasilia wa ukamilifu wake, na kwa hiyo, "hakuna awezae kuchagua mswada wowote miongoni mwa miswada hiyo na kuuamini kwa imani ya pekee eti mswada huo ndio wenye ukiritimba wa kuwa ndio maneno asilia ya watunzi."