Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha

Video: Mtanzania adaiwa kutekwa mchana kweupe huko Kibaha

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Inasemekana kwamba tukio limetokea jana (20.2.2025) majira ya saa saba mchana.Mkoa wa Pwani, Kibaha, Njuweni, sheli ya Puma.

Huyu kijana (boda boda) alikuwa anapambania maisha yake, akaomba msaada. Wananchi waliposogelea eneo la tukio, alishuka dereva wa hiyo Noah nyeusi ya watekaji akiwa na mtutu wa bunduki (kama inavyoonekana kwenye video), watu ikabidi warudi nyuma.

Boda boda akafungwa pingu kwa kusumbuana nao sana. Wakaanza kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Boda hakukubali kirahisi mpaka alipotolewa bastola na huyo aliyevaa vest nyekundu.




hilda.png

wate.jpeg


#########​

JamiiForums imewasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase kuhusu tukio hilo, amesema:

"Sina taarifa kamili juu ya tukio hilo, nami naliona tu, naomba mtupe muda tulifuatilie na tufanye uchunguzi wa kujua kilichotokea."

Soma:
 
Watanzania again, huyo kabaki peke yake hapo. Wanashindwa mkamata na ateswe aseme kisa cha kumteka, wanapompeleka? Hata simu yake kuikagua watu aliowasiliana nao, ingekuwa hatua nzuri ya kuanza nayo. Naona kingine, kutembea na silaha nowadays ni muhimu.
 
Back
Top Bottom