Mtibeli hebu funguka,
Hali kama hiyo ya mtoto kupigana na Baba yake ina sababishwa na nini hasa?
1. Mtoto wa kambo kukupasua ni Jambo unalotakiwa kulitarajia hasa akishaanza Kuota ndevu. Alafu ukiwa Una enforce laws and orders hapo home. Yeye ataona unamuonea mamaake.
Mara nyingi hiyo hutokea.
Kesi nyingi za Wababa kupigwa hutokea kwa watoto wakufikia(wakambo).
2. Mama kumdekeza na kumkania mtoto.
Mtoto ambaye hajadekezwa na Mamaake hawezi kupigana na babaake.
Baba anapotoa oda zake au kumuweka Sawa Mkewe, alafu mkewe akawa mkaidi na kuona anaonewa watoto hutokea kumchukia Mzee. Na hawawezi kukuelewa.
3. Mama kuwapa sumu watoto kwamba Baba Yao anahudumia wanawake wengine au anapenda familia nyingine kuliko wao
Chuki inayojengeka kwa mtoto hupekelea Mzee kupigwa mitama.
4. Mzee/Baba kuwa muonevu kupitiliza.
Baba linalewa mapombe, linakuja na kuanza kuleta ubabe wa kipumbavu,
Au kudhulumu haki za watoto.
Watoto wasio na uvumilivu hujikuta wakiwapa dawa, full doze Baba zao kuwaweka sawa.
5. Tamaa ya Mali.
Watoto wakishakuwa watu wazima. Kama ni vichaa kutoka kwa Mama zao. Walahi wabillah wanaweza kukuhujumu wakakuua.