Video na Picha: Ushahidi kuhusu yaliyotokea kwa Jaji Warioba wakati na baada ya vurugu, Ubungo Plaza

Video na Picha: Ushahidi kuhusu yaliyotokea kwa Jaji Warioba wakati na baada ya vurugu, Ubungo Plaza

Naona mmeanza kuupaka upepo rangi sasa! Makonda ndiye alieratubu vurugu hizo! Yeye na mdogo wake Nchemba anaeonekana hapo ndiyo chanzo cha Vurugu na kumpiga mzee wetu! Watoto hawana adabu hata kidogo! Laana ya wazee wetu itawadhuru hadi kwenye makaburi yenu ... Grrrrrrr

Hivi Maknda si ndio huyuhuyu aliyesema jaji warioba amezeeka anakaribia kufa? Kama sio yeye naomba aniwie radhi kwa kumchanganya na mtu mwingine.
 
Ujinga mtupu!

Sasa ni nini hiki? Mimi nilidhani hiyo clip itamwonesha mtu anayerusha jiwe. Kumbe kilichofanyika hapa ni TBC kuondoa picha ya Paulo Makonda wakati akimrushia jiwe jaji Warioba. Pathetic CCM.

Ningeshangaa sana kama TBC ingeweza kuonesha kitu kilichotokea wakati sasa chombo hiki kimebakia kuwa ni chombo cha propaganda cha CCM. Nchi ikirudi kwa wananchi, chombo hiki kinachokula kodi yenye bila faida yoyote itabidi kuvunjwa na kuanzishwa upya kikiwa na malengo mapya na maongozi mapya. Na nadhani uongozi wa juu uliokwishachafuliwa na CCM, wote itabidi kusafishwa.

Vipi kwani itv wameonesha makonda akimrushia warioba jiwe?
 
Mkuu nakwambia huyu Makonda ninatamani nimfanye kakondakita katika ile daladala yangu....yani amenichefua nafsi sana natamani awe hapa A town tumwonyeshee mambo!
Hahaha..mkuu, ipo siku atajichanganya huyu
 
Siku 70%ya watanzania wakijua ukwel itakuwaje?
Kabla ya kufikia hiyo asilimia 70 kwenye 50 tu hali itakuwa mbaya. Viongozi wengi wa chichiem watakuwa wanatembea kwa kujificha.
 
Kama huyu Makonda ni kweli alipanga mipango ya kuvuruga mdahalo, akafikia hatua mpaka ya kumpiga Mzee Warioba kwa mkono wake, laana kuu na iwe juu ya kichwa chake, na maiti yake inyofolewe na ndege kama ile ya Yuda Iskariote.

Kama ni kweli...!!!
 
Hapa CCM wanamteteaje Makonda mbona ushahidi uko wazi.
CCM acheni kujidanganya kuwa Warioba asome alama za nyakati wakati nyie ndo mnatakiwa msome. Nina uhakika event kama hii ikijirudia ndo mtajua nani wa kusoma alama za nyakati kati ya CCM na Warioba

Huo ushahidi ulioko wazi ni upi?
 
Jamiiforums is where we dare to talk openly!
Pix-4.JPG

Hapa no yupi!
 
Inawezekana vipi Tanzania ya 2014 watu washindwe kurekodi hata kwa simu tukio zima la kupigwa kwa warioba?

Dunia ya leo ya Twitter, youtube etc inamaana hata mtandao wa JF nao wameshindwa kupandisha hiyo video au ndio walikuwa hawana facilities za kurekodi kwa simu?

Alafu kuna watu wanatokwa povu kweli humu ndani eti makonda kampiga mzee warioba mara kamrushia chupa,,hiyo tv yao imeshindwa kuonesha ukweli wa hii habari sasa watu humu wanataka kutuaminisha kitu ambacho hakijatokea...
 
Watanzania tunapaswa kujifunza demokrasia ya kweli na kuvumiliana kwa maoni kinzani. Kilichotokea ubungo plaza ni ukosefu wa subira, utovu wa nidhamu, lakini kubwa ni kutoielewa vyema demokrasia. Walioingia na mabango walipaswa kuvumiliwa na kuacha waonyeshe mabango (mawazo) yao. Kisha kutolewa kwa amani. Hata hivyo nao walipaswa kupima hali. Wangetoa hayo mabango nje ya ukumbi au wakati wa mapumziko. Ikiwa walipanga kufanya fujo, hiyo ni shauri ingine. Ninashangaa vyombo vya ulinzi vilikuwa wapi kudhibiti haya!

Tatizo kuu ninaloliona ni kuwa pamoja na kuwa kwenye mfumo wa vyama vingi kwa zaidi ya miaka ishirini hatujawaandaa watu wetu kwa mabadiliko. Kuna watu wanaofikiri hakupaswi kuwa na mabadiliko ya kutawala na pale wananchi wanaposema na kutenda tofauti na mawazo yao wanalazimisha ya kwao. Tuwaandae wananchi jamani kuokoa taifa letu. Tumeyaona yaWaburkinabe tusifikiri sisi ni tofauti.

Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa sana, ule ulikuwa mdahalo huru unao accommodate fikra na mitazamo tofauti. Haukupaswa kujikita kwenye upande au kundi fulani, tafsiri ninayoipata ni kwamba kuna kundi fulani tu ndio lilipaswa kuhudhuria na kujadili, sifikiri kama ni sawa kujikita katika misimamo fulani bila kuwapa fursa ya kutoa maoni au kuonyesha imani zao watu wanaoamini tofauti na sisi. Msingi mkuu kabisa wa ustaarabu ni pamoja na uvumilivu, kuvumilia kusikia au kuona mambo tusiyopenda kuyasikia au kuyaona.

Ninafikiri kwa kuwa mdahalo uliandaliwa na taasisi inayohudumia watanzania wote, isingekuwa sawa kuhodhiwa na baadhi yetu huku tukiwafungia wapinzani wetu nje, inaleta picha ya kudhoofisha demokrasia jambo ambalo haliwezi kuleta afya kisiasa.
 
me namhurumia sana huyu mzee Warioba jamani yaani kama hii katiba itapatikana akiwa hai sijui
 
Warioba anapaswa kusoma alama za nyakati

Ccm kama mnadhani kumfanyia fujo na kuvuruga midahalo ya wana mageuzi ndio kujenga chama chenu,basi mtakuwa mnajidanganya.Wananchi wanajua sana hila za ccm na hukumu yenu inaandaliwa.
 
Bavicha kwa kupika majungu mmehitimu. Toka jana mnadai MAKONDA kampiga warioba lakini hakuna picha hata moja mliyoiweka zaidi ya ile inayoonyesha Makonda kasimama pembeni kama hatua 2. Hivi huo ukumbi hauna CCTV mpaka muambulie hiyo picha moja isiyo hakisi ukweli wa tuhuma? Hapo hakukua na watu wenye camera au smartphone wakapiga hizo picha za makonda anavyompiga warioba? Je hao washirika wenu wa Ukawa Itv ina maana wakati wanarusha kipindi hewani hawakuona hayo matukio ya kichapo?

Jaman hata kama mnapika majungu ifike hatua muwe mnajionea haya.

Hii inanikumbusha ya Soweto. Mbowe alisema ana mkanda na akaahidi kuutoa ili dunia nzima ishuudie ufedhuli wa ccm lakini mpaka juzi jeshi la polisi lilipowakamata watuhumiwa mbowe hakuwahi kuleta mkanda huo. Kwa maana nyingine Mbowe kakubali vijana wasiokuwa na hatia wafungwe wakati ushahidi kaukalia....

Hizi siasa zinatupeleka kubaya. Mwanzo tulikua na mwamko mkubwa na siasa za mageuzi lakini mpaka sasa wengine tulishakuwa na hofu kutokana na rangi za wanasiasa wetu.
 
Back
Top Bottom