Video na Picha: Ushahidi kuhusu yaliyotokea kwa Jaji Warioba wakati na baada ya vurugu, Ubungo Plaza


Hivi Maknda si ndio huyuhuyu aliyesema jaji warioba amezeeka anakaribia kufa? Kama sio yeye naomba aniwie radhi kwa kumchanganya na mtu mwingine.
 

Vipi kwani itv wameonesha makonda akimrushia warioba jiwe?
 
Mkuu nakwambia huyu Makonda ninatamani nimfanye kakondakita katika ile daladala yangu....yani amenichefua nafsi sana natamani awe hapa A town tumwonyeshee mambo!
Hahaha..mkuu, ipo siku atajichanganya huyu
 
Siku 70%ya watanzania wakijua ukwel itakuwaje?
Kabla ya kufikia hiyo asilimia 70 kwenye 50 tu hali itakuwa mbaya. Viongozi wengi wa chichiem watakuwa wanatembea kwa kujificha.
 
Kama huyu Makonda ni kweli alipanga mipango ya kuvuruga mdahalo, akafikia hatua mpaka ya kumpiga Mzee Warioba kwa mkono wake, laana kuu na iwe juu ya kichwa chake, na maiti yake inyofolewe na ndege kama ile ya Yuda Iskariote.

Kama ni kweli...!!!
 

Huo ushahidi ulioko wazi ni upi?
 

Alafu kuna watu wanatokwa povu kweli humu ndani eti makonda kampiga mzee warioba mara kamrushia chupa,,hiyo tv yao imeshindwa kuonesha ukweli wa hii habari sasa watu humu wanataka kutuaminisha kitu ambacho hakijatokea...
 

Nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa sana, ule ulikuwa mdahalo huru unao accommodate fikra na mitazamo tofauti. Haukupaswa kujikita kwenye upande au kundi fulani, tafsiri ninayoipata ni kwamba kuna kundi fulani tu ndio lilipaswa kuhudhuria na kujadili, sifikiri kama ni sawa kujikita katika misimamo fulani bila kuwapa fursa ya kutoa maoni au kuonyesha imani zao watu wanaoamini tofauti na sisi. Msingi mkuu kabisa wa ustaarabu ni pamoja na uvumilivu, kuvumilia kusikia au kuona mambo tusiyopenda kuyasikia au kuyaona.

Ninafikiri kwa kuwa mdahalo uliandaliwa na taasisi inayohudumia watanzania wote, isingekuwa sawa kuhodhiwa na baadhi yetu huku tukiwafungia wapinzani wetu nje, inaleta picha ya kudhoofisha demokrasia jambo ambalo haliwezi kuleta afya kisiasa.
 
me namhurumia sana huyu mzee Warioba jamani yaani kama hii katiba itapatikana akiwa hai sijui
 
Warioba anapaswa kusoma alama za nyakati

Ccm kama mnadhani kumfanyia fujo na kuvuruga midahalo ya wana mageuzi ndio kujenga chama chenu,basi mtakuwa mnajidanganya.Wananchi wanajua sana hila za ccm na hukumu yenu inaandaliwa.
 
Bavicha kwa kupika majungu mmehitimu. Toka jana mnadai MAKONDA kampiga warioba lakini hakuna picha hata moja mliyoiweka zaidi ya ile inayoonyesha Makonda kasimama pembeni kama hatua 2. Hivi huo ukumbi hauna CCTV mpaka muambulie hiyo picha moja isiyo hakisi ukweli wa tuhuma? Hapo hakukua na watu wenye camera au smartphone wakapiga hizo picha za makonda anavyompiga warioba? Je hao washirika wenu wa Ukawa Itv ina maana wakati wanarusha kipindi hewani hawakuona hayo matukio ya kichapo?

Jaman hata kama mnapika majungu ifike hatua muwe mnajionea haya.

Hii inanikumbusha ya Soweto. Mbowe alisema ana mkanda na akaahidi kuutoa ili dunia nzima ishuudie ufedhuli wa ccm lakini mpaka juzi jeshi la polisi lilipowakamata watuhumiwa mbowe hakuwahi kuleta mkanda huo. Kwa maana nyingine Mbowe kakubali vijana wasiokuwa na hatia wafungwe wakati ushahidi kaukalia....

Hizi siasa zinatupeleka kubaya. Mwanzo tulikua na mwamko mkubwa na siasa za mageuzi lakini mpaka sasa wengine tulishakuwa na hofu kutokana na rangi za wanasiasa wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…