Video na Picha: Ushahidi kuhusu yaliyotokea kwa Jaji Warioba wakati na baada ya vurugu, Ubungo Plaza

Video na Picha: Ushahidi kuhusu yaliyotokea kwa Jaji Warioba wakati na baada ya vurugu, Ubungo Plaza

Naona mmeanza kuupaka upepo rangi sasa! Makonda ndiye alieratubu vurugu hizo! Yeye na mdogo wake Nchemba anaeonekana hapo ndiyo chanzo cha Vurugu na kumpiga mzee wetu! Watoto hawana adabu hata kidogo! Laana ya wazee wetu itawadhuru hadi kwenye makaburi yenu ... Grrrrrrr
Atiiii...mdogo wake nani!?
 
Makonda anahusika kumtia ngwala mzee Warioba , hilo halina ubishi
 
Kikwete atakumbukwa daima kwa kuwaandaa, kuwalea na kisha kutusukumizia vichaa na kuwapa rungu! Naamini huko aliko anasikitika na kujilaumu.
 
Mag3,

..nilikuwa sijaona hizo BUNDUKI.

..sikuzoea kuona mtu amevaa KIRAIA halafu anabeba BUNDUKI.

..unaweza kudhani aliyefanyiwa vurugu ni Mzee Warioba peke yake,lakini walikuwepo Prof.Kabudi, Mzee Butiku, Mzee Awadh, Humphrey Polepole, na wajumbe wengine wa Tume ya Katiba.
 
Mag3,

..nilikuwa sijaona hizo BUNDUKI.

..sikuzoea kuona mtu amevaa KIRAIA halafu anabeba BUNDUKI.

..unaweza kudhani aliyefanyiwa vurugu ni Mzee Warioba peke yake,lakini walikuwepo Prof.Kabudi, Mzee Butiku, Mzee Awadh, Humphrey Polepole, na wajumbe wengine wa Tume ya Katiba.
Hivi prof Kabudi yupo? Nadhani akiulizwa kwa sasa lazima aseme hajawahi kufanyiwa fujo
 
Mag3,

..nilikuwa sijaona hizo BUNDUKI.

..sikuzoea kuona mtu amevaa KIRAIA halafu anabeba BUNDUKI.

..unaweza kudhani aliyefanyiwa vurugu ni Mzee Warioba peke yake,lakini walikuwepo Prof.Kabudi, Mzee Butiku, Mzee Awadh, Humphrey Polepole, na wajumbe wengine wa Tume ya Katiba.
Huwezi kuamini walipo kwa sasa wote hao uliowataja. Wapo waliopiga about turn na sasa wanakana msimamo wao wa awali na kwa usaliti wao huo wamezawadiwa! Kweli ndege wafananao huruka pamoja.
 
Huwezi kuamini walipo kwa sasa wote hao uliowataja. Wapo waliopiga about turn na sasa wanakana msimamo wao wa awali na kwa usaliti wao huo wamezawadiwa! Kweli ndege wafananao huruka pamoja.
Hata Mzee Butiku?
 
Kikwete atakumbukwa daima kwa kuwaandaa, kuwalea na kisha kutusukumizia vichaa na kuwapa rungu! Naamini huko aliko anasikitika na kujilaumu.

Atakuwa amepita ngazi hiyo ya "kusikitika na kujilaumu." Sasa hivi anasubiri tu yamfike mwenyewe. Ni kiasi cha muda tu, tuwe na subira.
 
Huu uzi wa mwaka 2014.
Kwa hiyo? Kwani wanaosemwa hawapo? Kwani vichaa wanaosemwa hawapo? Mbona wamejaa tele na wengine wamezidi kupewa marungu makubwa tu na wanayatumia vilivyo. Mitaani ni vilio tu rungu zikitembezwa!
 
Huwezi kuamini walipo kwa sasa wote hao uliowataja. Wapo waliopiga about turn na sasa wanakana msimamo wao wa awali na kwa usaliti wao huo wamezawadiwa! Kweli ndege wafananao huruka pamoja.

Hali hii ndio inayotumaliza kama taifa. Hatuna tena viongozi wenye msimamo thabiti juu ya jambo lolote. Hakuna wanaloliamini na kulisimamia. Hakuna 'conviction' juu ya jambo lolote isipokuwa ubinafsi wao pekee. Hiyo ndiyo CCM na viongozi wake wote.

Akina Makamba hata waone mabaya kiasi gani yakitendeka, watakaa kimya kulinda maslahi yao. Akina Nape, wameguswa, ndipo wanaanza kuona mabaya yanayotendeka kwa wananchi. Walipokuwa ndani walifungwa vitambaa vya macho wasione lolote baya. Akina Lowasa, Mwapachu, Slaa, oooh Slaa! Marehemu Sitta, Mwakyembe, Lipumba, Mrema, n.k. Kinana ataishi vipi na furaha ya kuona matunda ya kazi yake kubwa aliyoifanya kutufikisha hapa? Imani yake juu ya CCM ikawa muhimu zaidi kuliko taifa zima la Tanzania!

Mkapa, hivyo hivyo! Maprofesa wote waliowahi kuingia serikalini na waliomo sasa, na viongozi wengi ndani ya upinzani, msukumo ni ule ule, maslahi binafsi mbele kabla ya kulifikiria taifa linafaidika vipi! Kwa sasa namwondoa Lissu, Mnyika? kwenye orodha hiyo. Vijana wengine siwajui, na siwezi kuwahukumu.

Mwanzo nilidhani Magufuli angekuwa tofauti. Yeye amekuwa ni mtu wa kutaka asifiwe tu kwa njia yoyote ile hata kama ni kuumiza wasiomsifu. Yeye anataka awe kila kitu na lolote zuri lifanyikalo katika taifa hili ajulikana ni yeye aliyefanikisha. Taifa litaumia sana. Hajali taratibu wala sheria wala katiba ziko vipi. Sasa tunasubiri tu hadi 2025, kama ataamua na kutuhurumia atuache huru kama anavyosema.

Akiamua kufuata njia ya M7 na Kagame, basi tena!
 
1595363253707.png

MDAHALO wa kujadili Katiba inayopendekezwa ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere, jana ulivunjika baada ya kutokea vurugu ambako Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, alipigwa vibao shingoni na watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa CCM.

Hali hiyo ilijitokeza kwenye Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Ubungo Dar es Salaam, baada ya kuvunjika mdahalo huo uliokuwa umehudhuriwa na mamia ya watu, wengi wao wakiwa vijana.

Baada ya vurugu hizo, waandaji waliamua kuwatoa nje ya ukumbi wasemaji wa mdahalo huo akiwamo Warioba, Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, Profesa Palamagamba Kabudi na Profesa Mwesiga Baregu.

Wengine waliokuwa wazungumze kwenye mdahalo huo ni Humphrey Polepole na Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar, Awadhi Said, ambao wote walikuwa wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Warioba, aliyewahi kushika wadhifa wa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais, alipigwa vibao viwili shingoni alipofika kwenye mlango kuu wa kutoka ukumbini ambako kulikuwa na msongamano mkubwa wa watu. Wakati huo, Warioba na viongozi wenzake walikuwa wakitolewa nje ya ukumbi huo.

Hatua hiyo ilifanya mlinzi wake na baadhi ya watu waliokuwa wakimtoa kiongozi huyo waongeze mwendo na kumkimbiza kiongozi huyo wa taifa kwenye chumba maalumu cha wageni wa heshima (VIP lounge), kilichoko ndani ya hoteli hiyo.

Wakati Warioba akipigwa vibao, miongoni mwa watu waliokuwa karibu nyuna yake ni Katibu wa Uhamasishaji wa UVCCM, Paul Makonda.

Kwa sababu hiyo, baadhi ya vijana walichangia kumpiga kada huyo wa UVCCM aliyekuwa amevalia shati jeupe, huku wakimzuia kuingia kwenye chumba cha VIP ambako Jaji Warioba alikuwa amepelekwa.

Kufanikiwa kwa vijana hao kumzuia Makonda kuingia kwenye chumba hicho, kulitoa fursa ya kuendelea kupigwa hadi alipoponyoka na kukimbilia katika ofisi moja katika jengo hilo na kujifungia.

Baada ya kujificha katika chumba hicho, vijana hao waliitana na kuhamasishana ili wavunje mlango huo na kumtoa Makonda.

Hata hivyo baada kufanikiwa kuvunja mlango huo, vijana hao hawakumuona Makonda hadi walinzi wa hoteli hiyo na askari kanzu walipofika hapo na kuwafukuza.

Vurugu zilivyoanza

Vurugu katika mdahalo huo zilianza muda mfupi kabla ya Jaji Warioba aliyekuwa msemaji wa kwanza, kumaliza hotuba yake.

Baada ya kumaliza kuichambua Katiba inayopendekezwa, Jaji Warioba alisema katika kuitetae katiba hiyo, baadhi ya watu wamekuwa wakimtumia Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere kuunga mkono hoja zao.

“Tunatumia jina la Mwalimu ili kuunga mkono hoja zetu wakati mwingine ninajiuliza hivi tunatumia Mwalimu yuleyule ama…

“Mwalimu amekufa akisema hajaona hata sehemu ya kutia koma katika Azimio la Arusha, kuna watu waliwahi kumletea Mwalimu barua wakimwambia afungue akaunti nje ya nchi ndiyo fedha zake zitakuwa salama… Mwalimu siyo tu alikataa lakini alitangaza kila kitu hadharani.

“Leo Mwalimu angekuwapo angekubali watu wafungue akaunti nje ya nchi, angekubali watu wapewe zawadi wakae nazo… nikasema huyo wao siyo Mwalimu, Mwalimu alikuwa ni mtu mwenye uwezo wa kufanya uamuzi mgumu hata unaomhusu yeye,” alisema Warioba.

Vijana na mabango

Baada ya maneno hayo, baadhi ya vijana takriban 20, walisimama na kunyanyua juu mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali wa kumtukana Jaji Warioba na mengine yakisifu Katiba inayopendekezwa.

Kitendo hicho kilifanya baadhi ya watu kujaribu kuwakalisha chini huku wengine wakichana mabango hayo hali iliyozusha vurugu.

Wakati wote huo Jaji Warioba alikuwa amesimama akijaribu kuwasihi watu hao kukaa chini, lakini hali hiyo ilionekana kutozaa matunda.

Baada ya muda vijana hao walijitenga pembeni karibu na jukwaa kuu huku wakiwa na mabango yao, wakiimba nyimbo mbalimbali za CCM.

Hali hiyo ilisababisha baadhi ya watu watoke ukumbini huku wengine wakiwa wanarudi kuketi kwenye viti vyao.

Wakati vurugu hizo zikiendelea, Profesa Kabudi na Butiku kwa nyakati tofauti, walionekana wakimtaka Makonda kuwatuliza vijana hao wa CCM ambao alidaiwa yeye yeye ndiye aliwaingiza katika ukumbi huo.

Wakati viongozi wakimtaka Makonda kufanya hayo, vijana wengine walionekana kumvuta Makonda wakitaka kumpiga hali iliyomlazima kumtumia kama kinga, Amon Mpanju, ambaye alikuwa Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba akiwakilisha kundi la walemavu.

Hali iliendelea hivyo hadi baadhi ya vijana waliokuwa wamekaa walipohamasishana na kuwapiga wale waliokuwa na mabango, kwa kutumia viti hali iliyofanya wakimbie na kutoka nje ya ukumbi huo.

Baada ya vijana hao kutoka nje, hali iliwageukia Makonda na Mpanju ambao baada ya kuona hali imekuwa tete, walikimbilia kwenye jukwaa kuu na kukaa karibu na Jaji Warioba.

Huku hali ikiwa bado ya taharuki, viongozi hao (Warioba na wenzak) waliamua kutoka nje ya ukumbi na ndipo zahama ya kupigwa vibao kwa Jaji Warioba ilipojitokeza.

Wahuni wampiga Jaji Warioba Dar - Mtanzania
 

Attachments

  • 1595362539734.jpeg
    1595362539734.jpeg
    22.9 KB · Views: 4
Back
Top Bottom