Nachukia ukoloni na katu siwezi kuonea ufahari ujaji wa Wakoloni barani Afrika! Hata hivyo, hiyo hainiachi kuwaza kwamba je; huenda kama si ujaji wa Wakoloni Afrika; hivi sasa si ajabu bado tungekuwa kwenye primitive life kama hao?! Tungekuwa tumepiga hatua kiasi gani?
Anyway, sijasoma history... ngoja weekend hii nitumie muda kidogo kujisomea yale ambayo niliyasikia nikiwa Form I & II... Zama za Kale za Mawe; Ugunduzi wa Moto n.k! Ningependa kufahamu wakati Mswahili anaweza kuchonga jiwe kwa kutumia mawe; makabila mengine (non Africans; white in particular) walikuwa wapi!
Nikirudi kwenye mada; interest yangu sio "Waafrika" hao kwenda India... bali ni nini kiliwafanya ku-risk maisha yao kiasi cha kuingia kwenye mitumbwi hadi India! Let's wanatoka Tanga... walipokuwa wanaishi pakakumbwa na disease outbreak na hivyo kuwa si salama tena kuishi!! Kwanini wali-opt kuelekea Eastwards hadi baharini na kuanza kukata maji bila kufahamu wanaenda wapi.... huku nikiamini hawakuwa na mitumbwi ya kuweza kuhifadhi idadi kubwa ya chakula na maji... by the way; wangehifadhi kwa kutumia vifaa gani?! Why instead moving eastwards, hawakuelekea north/west/southwards ambako wangeweza kulikimbia eneo hatarishi bila ku-risk maisha yao tena wakiwa na uhakika wa kupata chakula kwavile wangekuwa wanasafiri pori kwa pori!!!!
Hebu nikumbusheni wataalamu wa historia! Wale Wangoni wa Kusini mwa Tanzania ni moja ya sehemu ya Wazulu ambao kusafiri kwao northward to Tanzania ilitokana na civil wars kule kwao?!
Mkuu
Copenhagen DN, kwa hii ID yako naweza ku-assume upo Denmark! Kama ndiyo, kuna motivation factor iliyokufanya ku-move northward to Denmark! Kutafuta elimu, maisha na mambo mengine kama hayo! Nini inaweza kuwa motivation factor ya hao watu?!