Video: Nabii Olivia asikika akimpanga muumini apige kelele kuashiria anatolewa mapepo

Biashara kama zingine tu ila hii ni mbaya zaidi hata kiuchumi, mijamaa haifanyi kazi, Ulongo Ulongo tu daily, wajinga wao wakiwachangia.
Wangefanya kama Rwanda tu wayafute makanisa yote ya dizaini hii,eti nabii sketi aliyovaa tu ni aibu imebana kama wanawake wanaojiuzaga mjini ni upumbavu wa hali ya juu kabisa
 
Mbona sijaona kitu kama kupangwa katika video zaidi ya utani wa Dj Choka naye akijifanya anaombea mapepo kwa mdada. Lakini wadau walivyocomment sasa ???!!
 
Mbona sijaona kitu kama kupangwa katika video zaidi ya utani wa Dj Choka naye akijifanya anaombea mapepo kwa mdada. Lakini wadau walivyocomment sasa ???!!
Sikiliza vizur pale anaposema "mpe Amani huyu msichana" baada hapo ukiskiliza vizuri ndo anamwabia "lia kwa nguvu, " piga kelele" halafu hata kama hujaskia matendo tu ndo yanaonesha hivi MTU aloanguka na majini asimame mwenyewe baada ya sekunde?? Na alivokuwa anakung'uta nguo utafikiri jini mahaba yupo kwenye Nguo, Aisee Mungu awasamehe tu
 
Ndio mana na hapa bongo, kamanda Magu anatakiwa awashikishe adabu ka alivyofanya mzee mzima Kagame. Fungia makanisa yote yalokaa kilongolongo.
 
Madame Olivia naamini unasoma thread hii ushauri wangu kwako ni kutubu mbele za Bwana kwanza kwa hayo yaliyotukia kwa sababu Kanisa la Kristo limetukanwa, nyenyekea mbele za Mungu na mwambie Roho wa Bwana akusaidie uende hatua hata hatua katika wito na huduma aliyoweka ndani yako. unajua kila calling ya Mungu inakwenda kwa hatua na kwa maongozi ya Roho wa Yesu.unahitaji experience ya kutosha katika kutembea na Bwana kabla hujaanza kupost video kwenye Youtube na mahali penginepo kwenye mitandao ya jamii.

Unahitaji kuendelea kutulia chini ya baba wa kiroho na kujifunza mpaka utakapokua tayari umeiva kwa wito wako..kila ngazi za kiroho zina changamoto zake,upako ulionao bado haujatosha kufanya unachofanya na ndio maana umepata kashfa na dhihaka zote hizo
tulia tulia tulia ...!!! Mungu atakuinua na kukufikisha unapotamani kwa wakati wake..
sikiliza mafundisho ya Mwalimu Mwakasege na haswa ya tarehe 8/3/ 2017 yatakusaidia..amefundisha vizuri sana juu ya kutulia kwa Mungu ili aweze kukusaidia kufikia pale Mungu alipokusudia

naamini ushauri huu utakusaidia
 
Siku hizi wamechonga lonasanamu jeusi ili kuonesha nalo ni li-Afrika
 
Nimeona clip nyingine eti anaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kwenye hiyo video ya maombezi. ......

Eti ni kitu amekuwa akifanya muda mrefu....

Pia hili limetokea kwa sababu Mungu ameamua watu wengi wenye shida waende kanisani kwake kuombewa
Lijinga sana hili limama. Nimeona hiyo clip. Linajitetea eti alimwambia yule mwanamke alie kwa nguvu ili kuondoa uchungu alionao moyoni....[emoji21] [emoji21] .
Wakati hoja haikuwa uchungu moyoni bali alikuwa anafukuza jini mahaba!!. Ama kweli wakristo ni wajinga. Hata hiyo nayo hamgundui kuwa uongo?
 

Aaaaah, wacha bwana.

Mbona sijaiona hiyo clip mkuu. Hebu fanya kuitupia hapa jamvini au tayari upo uzi unazungumzia hiyo video kiongozi...?
 
" lia kwa nguvu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji15] [emoji15]
Ni sehemu ya kuhamasisha neno. Mbona wasanii wa bongo fleva huwa wanasema Piga keleleeeee! Na watu wanapiga kelele kweli. What is the difference. Kwanini wasijipigie kelele wenyewe mpaka waambiwe?
 
Mimi ni mkristo lkn dini ya kiislam naikubali sana
hainaga mambo mengi.
kitendo cha korani kuiacha kwenye lugha mama ya dini ilikuwa na maana kubwa sana. ni vigumu mtu kuingiza mbwembwe zako kihuni wakati unahubiri. safi sana kwa hilo.
 
kitendo cha korani kuiacha kwenye lugha mama ya dini ilikuwa na maana kubwa sana. ni vigumu mtu kuingiza mbwembwe zako kihuni wakati unahubiri. safi sana kwa hilo.
Yasingetokea madhehebu kama hilo tu, lingetosha kuuacha ujumbe wake wa asili ufike. Hazibatilishwi ktk maandishi bali tafasiri zake ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…