Madame Olivia naamini unasoma thread hii ushauri wangu kwako ni kutubu mbele za Bwana kwanza kwa hayo yaliyotukia kwa sababu Kanisa la Kristo limetukanwa, nyenyekea mbele za Mungu na mwambie Roho wa Bwana akusaidie uende hatua hata hatua katika wito na huduma aliyoweka ndani yako. unajua kila calling ya Mungu inakwenda kwa hatua na kwa maongozi ya Roho wa Yesu.unahitaji experience ya kutosha katika kutembea na Bwana kabla hujaanza kupost video kwenye Youtube na mahali penginepo kwenye mitandao ya jamii.
Unahitaji kuendelea kutulia chini ya baba wa kiroho na kujifunza mpaka utakapokua tayari umeiva kwa wito wako..kila ngazi za kiroho zina changamoto zake,upako ulionao bado haujatosha kufanya unachofanya na ndio maana umepata kashfa na dhihaka zote hizo
tulia tulia tulia ...!!! Mungu atakuinua na kukufikisha unapotamani kwa wakati wake..
sikiliza mafundisho ya Mwalimu Mwakasege na haswa ya tarehe 8/3/ 2017 yatakusaidia..amefundisha vizuri sana juu ya kutulia kwa Mungu ili aweze kukusaidia kufikia pale Mungu alipokusudia
naamini ushauri huu utakusaidia