PostGE2025 Video: Ndugu wa walioshtakiwa kwa Uhaini baada ya Uchaguzi wafurika Mahakamani

PostGE2025 Video: Ndugu wa walioshtakiwa kwa Uhaini baada ya Uchaguzi wafurika Mahakamani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Leo Novemba 19, 2025 kesi za uhaini zinazowakabili washtakiwa zaidi ya 100 (waliokamatwa kwa nyakati tofauti kuanzia Oktoba 29) zinatarajiwa kuendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo ndugu na jamaa wa washtakiwa, waliofika mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza kesi za ndugu zao wameelezwa kuwa washtakiwa hawatoletwa mahakamani na kesi hiyo itaendeshwa kwa njia ya mtandao.

Wakili Sisty Massawe ambaye yupo kwenye jopo la Mawakili wanaowatetea washtakiwa amewaeleza ndugu taarifa hiyo huku akiwataka kuwa wavumilivu wakisubiri amri ya mahakama.

 
Back
Top Bottom