Video: Ni kweli kina cha maji kimepungua sana kwenye matanki ya Mto Ruvu?

Maji yapo mengi sana Tanzania huko Mbeya, Arusha na Kilimanjaro yanamwagika hovyo kwenye mitaro China wametoa maji zaidi ya 800km kwenda kwenye jimbo lingine sisi tupo busy kushangilia Uchaguzi kila baada ya miaka mitano na kununua magari ya washawasha huku tukiwa hatuna maji ya kutosha kwenye miji mikubwa...
 
Miaka ile mbeya wale DANIDA walipokuwa wanafanya mradi ule jamaa walikuwa wanafanya kwa uweledi mkubwa mpk wakafanikisha zoezi lile
Maana maji yanakusanywa sehemu mbali kutoka kwenye vyanzo na wanayaingiza kwenye matank makubwa

Ova
 
Nafikiri ipo haja ya kuanza kufikiria kusafisha maji ya bahari/kuyatoa chumvi yatumike kwa matumizi ya nyumbani (kama mbadala kipindi cha kiangazi). Hiyo process kwa kitaalam huitwa "Desalination"

Tunaweza kuomba hiyo technologia huko Saudi Arabia ambapo wanaitumia kwa ufanisi na kwa miaka mingi... pengine wakatusaidia bure kwani wanapenda kusponsor miradi ya maji.

Nchi nyingine maarufu kwa hiyo technologia ni; United Arab Emirates, Israel, Kuwait, Australia, Spain nk
 
Mbeya kwenyewe maji bado yanatoka kwa mgao
 
Desalination changamoto yake ni ile chumvi unayoichuja unaipeleka wapi, ukiidump ardhini unaharibu mazingira, ukiidump baharini with time unaongeza concentration ya chumvi baharini unadisturb ecosystem ya viumbe majiโ€ฆNa pia ni expensive kurun!!..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ