Cannabis
JF-Expert Member
- Jan 20, 2014
- 11,557
- 33,535
Kama inavyoonekana kwenye video hapo, wimbo huu umekuwa ukileta hamasa kubwa sana kwa wananchi pale unapopigwa kwenye kampeni za mgombe Rais kupitia CHADEMA Mh. Tundu A. Lissu.
Wimbo huu unatuma ujumbe wa muungano na upendo katika kipindi ambacho tunapitia changamoto kubwa ya siasa za chuki na uadui. Tetesi nilizoambiwa wimbo huu kwa sasa ni marufuku kupigwa katika vyombo fulani vya redio ili kutoonyesha kuunga mkono upande fulani mpaka kipindi hiki cha uchaguzi kitakapopita.
Nawakumbusha watanzania wote tukapige kura pamoja with "one love", tumchague kiongozi atakayetupa furaha na maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.