Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,822
Rais wa Jamhuri ya Kenya amekubali kushindwa....
Amekubali kuwa yeye ni kiongozi wa serikali lakini kubwa zaidi ni kiongozi wa wananchi wa Kenya...
Amekubali kuwa sauti ya umma ni sauti ya Mungu...
Amekataa na kutambua kuwa uongozi si kutumia nguvu na mabavu bali ni kuwa na sikio la kusikiliza, kuelewa na kutatua changamoto za watu...
Amekataa ujinga na upumbavu wa viongozi wengi wa Afrika ikiwemo Tanzania kudhani kuwa watakaa milele kwenye dhamana za madaraka na uongozi walionao sasa...
Wa hapa kwetu Tanzania (Rais Samia Suluhu Hassan) kwa jinsi alivyolewa madaraka alishajisahau kabisa kuwa leo yupo pale lakini hajui kuwa pengine baadae kidogo au kesho atakuwa hayupo kwenye nafasi hiyo.
Hana sikio la kusikiliza na kuelewa. Kama ana masikio, basi husikia lakini huwa haelewi...
Akielewa, basi huelewa vibaya kwani mwisho huishia kurusha vijianeno au vikauli vyenye ukakasi wa kashfa ndani yake kwa waliompa dhamana hiyo ya uongozi na huoesha wazi kuwa hata hajui dhamana ya madaraka ya nafasi ya u - Rais wa nchi aliyonayo...
Mara yingi amejiita yeye ndiye "CHAWA MKUU" na kuunda vikosi vya CHAWA kumtetea..
Na siku chache zilizopita amejiita yeye ni "CHURA KIZIWI" asiye sikia na hivyo hata kuelewa hawezi kuelewa anaowaongoza wanataka nini na wana hisia gani dhidi ya uongozi wake maana yeye ni chura asiye na masikio..!!
Yeye na wenzake waelewe hili: Mabadiliko yanakuja iwe ni kwa HERI au kwa SHARI. Bora wakawa na akili kuyapokea mabadiliko hayo kwa heri kabla shari haijawakuta..!