Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 3,092
- 5,386
Admins. Naona mnaondoa hizi Videos ambazo zinazungumza kwa ushahidi na wala si kashfa wala matuzi. Leo admin uliyepo ni yupi ambaye hutaki ukweli? Hakuna matusi wala kashfa.
View attachment 3160236
Tukianza kuposti kila kinacho ongewa na wanaojiita Manabii/ Mashehe/nk nk nk nafikiri tunaweza kutoka nje kabisa ya Dini. Muhimu kila mtu ASOME (SOMA, SOMA, SOMA kuepuka taarifa potofu!!! Hivyo naunga mkono kudelete hoja za hovyo hovyo zinazolenga dini yoyote huku majukwaani....
Kwa upande wa mada iliyo mezani;
Kwa upande wa Uislam; maana ya Uislam ni Kunyenyekea kwa Mungu mmoja, asiye na mshirika na asiyefanana na kitu chochote lakini pia kutii na kufuata mafundisho ya Quran yaliyofikishwa kwa binadamu kupitia kwa mitume wa Mungu.
Ukisikia habari yoyote juu ya Uislam unatakiwa uone kama ina reference yoyote ya Qurani au ya mafundisho ya mitume wa Mungu, tofauti na hapo, yaweza kuwa ni mawazo binafsi kutokana na uelewa wa mtu