Video shooting and editing company

hurrem_sultana

Senior Member
Joined
Sep 6, 2018
Posts
136
Reaction score
361
Habari za wkend wakuu

Mda umefika wa mimi ku own kampuni yangu sasa,nimekaa nimejitahidi kuangalia ideas mbali mbali ila nikaona hii ya video shooting/editing itanifaa zaidi kwa sababu pia ina relate na fani yangu niliyosomea ya IT itakua rahis ku catchup vitu na kuindesha kwa ufasaha zaidi pia kitu kingine biashara hii unaweza ukaichanganya kwa pamoja na upigaji picha,utengenezaji wa mabango,logos,na vitu vinavyo relate na hvyo.nilikua na ideas mbili kichwani hii niliyoandika hapa na restaurant & fast food ila naona hii ikae pembeni kwanza ina risk nyingi kiasi.

Nimekujaa hapa wakuu naomba ABC za hii biashara ya video shooting,editing and picture taking.soko langu kubwa najua itakua maharusi,vipaimara,sendoffs, event mbali mbali n.k..nataka kujua mahitaji yote ya vitu na vifaa vinavyohitajika,nitawatafuta wataalam pia kujua zaid ila nataka nianzie hapa kujua abc za mambo haya

Asanteni sana
 
Fanya jitihada zako ujue hiyo ABC ili hapa angalau upewe DEFJ... Maana usiombe unashauriwa afu huna pakucompare huwezi jua upi mchele ipi ni pumba..!
 
Fanya jitihada zako ujue hiyo ABC ili hapa angalau upewe DEFJ... Maana usiombe unashauriwa afu huna pakucompare huwezi jua upi mchele ipi ni pumba..!
Hata kuja hapa ni moja ya jitahada tena kubwa sana kwasababu pana mkusanyiko mkubwa na unaweza kukuta hata wenye kampuni kama hizo wapo humu humu
 
1. camera nzuri za video , kwa kuanzia angalau 2.. canon 5d mark 4 zinatumika sana na wengi
2. light kit, taa za video za kutosha.. kuna ring right, led light, kubwa na ndogo za kufungwa kwenye camera
3. computer nzuri ya kuediti kazi.. wengi wanatumia mac, zenye ram kubwa not less than 8gb, processor kubwa ya kisasa, etc
4. flat screens angalau 2 za kuanzia na projector 2 zenye lumens kubwa.. not less than 3500 lumens.. ukumbini kwenye masherehe lazima uwe na video displays kubwa kuonesha tukio
5. eneo au ofisi ya kufanyia indoor shoot, iwe ya video au kupigia picha.

6. camera za kupigia picha angalau 2, wengi wanatumia nikon full frame yeyote inafaa
7. vikorombwezo vya camera ya picha, kama speedlights, lenz za size tofauti tofauti, etc

kwa kuanzia ni hayo tu... mengine ni knowledge kubwa sana ya kushoot na kuedit picha na video

hivyo ndivyo nilianza navyo.. na ndivyo muhimu sana.. vingine nakuwa nakodi tu nikiwa na kazi yenye mahitaji makubwa

by ceo wa mobile studio mabibo hostel (@photo_studio_mabibo_hostel) • Instagram photos and videos
 
Asante sana mkuu hakika wewe ni mtu mwema,vipi biashara lakini ina return nzuri?
 
biashara zote duniani zinalipa.. tofauti ni mbinu zako tu kupata wateja,,, kuna watu wanatajirika kwa boda boda na kuna watu wanafilisika
Asante sana lazima niandae mipango makini ya kujitangaza na kupata kazi nyingi haswa za wachagga.

Naomba nikuulize one more question mkuu,kwa uliyonitajia hapo at least niwe na kiwango gani cha kuanzia na kubuy hayo mahitaji yote ya kuanzia?
Roughly approximation
 

milion 15 hadi 20

gharama kubwa ni camera na lenzi tu.. vingine havitishi sana, labda na computer ndio bei
 
Naipenda hii biashara,muhimu ubunifu na uaminifu kwa vijana wako utakaokuwa nao ila ina return nzuri,mbali na hvyo kuwa na vifaa bora vya kazi
 
kutumia hizo camera niliacha muda... now days ni dslr au miror less camera.

hizo camcoder quality yake ya kizamani sana.. na lenz zake hazina flexibility kama dslr.

kama upo serious unataka quality work nunua canon 5d mark 3 au mark 4.
Katika sehemu nilipokuja kujua hujui lolote kwenye hii tasnia ni kwenye hiki ulichoandika hapa. Kha...so sad

Unasema camcoder quality ya zamani? Hiiiiiii, hv izo tv tunazoangalia kila siku studio wanatumia dslr? [emoji23][emoji23][emoji23]

Kwanza DSLR tunatumia kwenye matukio mafupi mafupi kama ku shoot movie za kibongo, muziki nk kwakuwa dslr hata iyo 5d mark 4 haina clip ya lisaa limoja mfululizo, dslr zinachemka, clip zina time limit, not flexible on handling kwa matukio ya ku move na nyingi zina focus struggle

Camcoder ndio maalumu kwa video, ina fast focus, inaweza shoot hata masaa matatu mfululizo bila ku heat wala kuwa na limitation. Sasa kachukue DSLR yako sijui Mark IV kashoot harus kanisani kisha uende nayo ukumbini pia ukashuti masaa manne. Kama hutopigwa mawe na wenye mkanda kwa kumis matukio.

Ushauri wangu kwa muuliza swali
Tafta Camcoder kwa kazi kubwa. Na zina uwezi wa video kuliko dslr. Tafuta DSLR kwaajili ya short shooting, photos in and out doors, movies zenye script, au matukio yenye script, lakini sio mengineyo. Sio non stop or continuous events
 

inawezekana ukawa sahihi wa upande wako.. ila kwa experience yangu dslr ndio best choice zama hizi..sababu ya flexibility... nimebahatika kuwa na access na studio kubwa nyingi wakati najifunza kazi.. from kwetu studios, iview studios mpaka clouds tv.... dslr ndio zinatumika sana zama hizi.

ila wewe usiwe mbinafsi.. badala ya kuniponda mimi... ulitakiwa umshauri huyo dada juu ya swali lake kama mimi nilivyomshauri.... umeona kuniponda mimi ni ujanja kuliko kumsaidia mtoa mada.. apate majibu ya swali lake mazuri..

usiwe na roho hiyo ya kwa nini..mimi sijaomba ushauri wowote.. tumia uzoefu wako kuwasaidia wanaouliza maswali... wapate ushauri mzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…