Video: Si rahisi "dictatorship regime" yoyote kuruhusu watu kama hawa waishi katika nchi wanazoongoza

Video: Si rahisi "dictatorship regime" yoyote kuruhusu watu kama hawa waishi katika nchi wanazoongoza

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Hii ilikuwa katika bunge la pili la Utawala wa Mwendazake mwaka 2017 (mwaka mmoja na nusu hivi baada ya Magufuli kuingia madarakani). Miezi michache baadaye mbele akapigwa risasi kadhaa ili afe. Hakufa.

Ukiitazama na kusikiliza madini kama haya toka kwa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida Mashariki Tundu Lissu, unaweza kuelewa ni kwanini "kikuza sauti" cha "baraza kuu la wananchi" hampendi na bila aibu huonesha chuki za waziwazi kabisa kwa mtu huyu.

Unaweza kuelewa pia ni kwanini huyu ndugu alikuwa "sumu hatari" chini ya utawala wa Mwendazake kiasi cha mkakati hatari wa kum - eliminate mazima mwaka 2017 ukasukwa huku "kikuza sauti" cha chombo kile akitumika kisawasawa kufanikisha mpango huu mbaya kabisa.

Tazama na sikiliza mwenyewe halafu ukiweza, sema kitu.


Huyu jamaa alikuwa mleta taharuki sana kwenye kambi ya wapinzani wake CCM na serikali. Tazama picha vizuri utaona wafuasi Wa Mwendazake ndani ya jumba lile wanavyozungusha shingo kwa taharuki wasielewe jamaa kaujuaje uzembe na uongo wao.

Kwa kifupi kabisa tunaweza kusema HII NDIYO KAZI YA MBUNGE MAKINI.
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta

Bavicha wote sasa hivi wanashangilia ccm
 
Mafanikio ya Samia ni habari mbaya sana kwa Lisu maana 2025 hana chake tena.

Ccm itaendelea kupeta

Bavicha wote sasa hivi wanashangilia ccm
ACHA blabla wewe, twende na tume huru, katiba mpya then wananchi wafanye maamuzi yao nani awe kiongonzi wao , shida iko wapi ,mbona sioni shida
 
Madikteta hawapendi watu timamu wanaohoji vitu nyeti !

Ndio maana ukianza kuona vyombo vya habari vinadhibitiwa ujue ni dalili za udikteta !madikteta na vyombo vya habari hawapatani


Bunge likazimwa eti watu wafanye kazi ila dikteta akitaka kupita masaa 4 watu wanapangishwa foleni hadi apite!
 
Back
Top Bottom