(VIDEO) Songwe: Wanaochimba nguzo za umeme wakutana na masalia ya mwili wa mtu kwenye shimo

(VIDEO) Songwe: Wanaochimba nguzo za umeme wakutana na masalia ya mwili wa mtu kwenye shimo

Wakazi wa eneo la Old Vwawa mkoani Songwe wamekutana na kinachodaiwa kuwa ni mabaki ya binadamu katika shimo ambalo lilichimbwa maalum kwa ajili ya kusimika nguzo.

Shimo hilo lipo eneo hilo katika mradi wa kuweka nguzo za umeme kutoka Old Vwawa kwenda Msambawani mkoani hapo.

Mmoja wa mashuhuda katika eneo la tukio amesema kuwa baada ya kuchimba shimo hilo wachimbaji wakakuta vitu kadhaa walivyovitaka kuwa ni masalia ya mwili wa binadamu.

Baada ya kutafutwa leo Jumatano Machi 2, 2022 msimamizi wa mradi huo katika eneo la tukio, Nickson Albert akasema:

“Mimi ni kiongozi wa mradi kwa eneo hili, ni kweli sikuwepo wakati wanachimba hilo shimo, lakini nilipofika hapo wakasema wamekuta mifupa ya binadamu, cheni, bangili na vingine kadhaa.

“Inaonekana ni mwili wa miaka mingi lakini ajabu bado vitu vimekutwa katika mazingira ambapo havijaharibika sana.

“Mradi huu wa nguzo unatoka Old Vwawa unaenda Msambawani, hivyo vitu vilitolewa na kufikishwa kwa viongozi wa Serikali za mtaa ambao hawakutilia manani.

“Hadi sasa shimo halijafukiwa wala kuwekwa nguzo, hivyo vitu vimehifadhiwa na wachimbaji kwa kuwa hakuna jitihada zozote za mamlaka kuchukua hatua za ziada.

“Nimeshawasiliana na viongozi wangu wa juu ambao hawapo eneo la tukio, wamesema watakuja kwa ajili ya kujua kinachoendelea.”

Katika video ambayo wachimbaji wamerekodi wakati wakitoa hivyo vitu kwenye shimo wanasikika wakieleza kuwa mwili huo utakuwa ni wa mwanamke kwa kuwa wamekuta bangiri, cheni, jino na mifupa.

View attachment 2136360
View attachment 2136361

4F963055-FB97-4495-9E72-0CDB0771ED0E.jpeg
 
Duuh Damu ya mtu nzito Sana
Kama walimuua kinyemela basi na wakamzika kinyemela basi ishajulikana

Note; mwili wa binadamu unauwezo wa kukaa miaka zadi ya 3 chini ardhi ndiyo unaoza sasa huyo inaonesha aliuwawa muda mlefu sana
Unaweza kuta aliyeuwa nae alishakufa
 
Mbona mnakazana kua kauwawa, si ajabu alizikwa maana hicho kishimo ni kirefu.

Kuna watu hawajari makaburi ya wapendwa wao, matokeo yake zile alama kua hili ni kaburi huwa zinapotea kabisa na kubaki kama shamba tu.

Huenda hapo palikua ni kaburi la huyo mti ila lilitelekezwa na labda shamba likauzwa na kuuziana mpka tanesco wakalikuta.
 
Duuh Damu ya mtu nzito Sana
Kama walimuua kinyemela basi na wakamzika kinyemela basi ishajulikana

Note; mwili wa binadamu unauwezo wa kukaa miaka zadi ya 3 chini ardhi ndiyo unaoza sasa huyo inaonesha aliuwawa muda mlefu sana
Ikibidi wakazi wa mkoa huo wenye historia ya kupotea kwa ndugu zao wa kike waombe hivyo viungo wakafanye DNA test wafanye matanga ya ndugu yao.

Inawezekana wapo watu wanamsubiri ndugu yao atarudi alienda kutafuta maisha kumbe alishakuwa marehemu kitambo.
 
Duh kazi kweli isje kuwa nao wamechimba kaburii...[emoji848][emoji2955][emoji2955]
 
Ikibidi wakazi wa mkoa huo wenye historia ya kupotea kwa ndugu zao wa kike waombe hivyo viungo wakafanye DNA test wafanye matanga ya ndugu yao.

Inawezekana wapo watu wanamsubiri ndugu yao atarudi alienda kutafuta maisha kumbe alishakuwa marehemu kitambo.
Hapo ndipo Mungu anapoonyesha uwezo wake
Binadamu tumekuwa katili Sana
Yaani ukute Chanzo pesa au Mapenzi
 
Kwanza wamekosea sana kuchukua hayo masalia ya mwili wangeuacha hapo then police wake waweke utepe wachukue mwili wote uliobaki wapeleke kwenye forensic investigation wachukue DNA halafu mwili uhifadhiwe pahala then itangazwe watafutwe ndugu ambao wataweza kutambua hizo bangili na wapimwe DNA kwa ndugu wanaoclaim kwamba ndugu yao aliwahi kupotea hawakujua amekufa au mzima.

Then baada ya hapo file la upelelezi wa kifo lifunguliwe na upelelezi uanze maana itajulikana tu Mara ya mwisho alikuwa na nani especially huko vijijini ni easy wanajuana.

Huu uzembe mkubwa sana kwa police
 
Ndo maana wafanya kazi wa tanesco akili hawana.
Kila siku wanachimba makaburi na kuzika nguzo.
Kuna kazi zinalaana
 
Duuh Damu ya mtu nzito Sana
Kama walimuua kinyemela basi na wakamzika kinyemela basi ishajulikana

Note; mwili wa binadamu unauwezo wa kukaa miaka zadi ya 3 chini ardhi ndiyo unaoza sasa huyo inaonesha aliuwawa muda mlefu sana
Unadhani wahalifu watakamatwa!!??
Pengine nao walishadedi
 
Back
Top Bottom