kilam
JF-Expert Member
- Aug 5, 2011
- 2,092
- 2,128
Mara nyingi huwa nakupuuza maana huwa haupo tayari kujadili mada yoyote, huwa unarusha majibu bila kutumia akili au walau kujaribu kutafakari na kudhihirisha uwezo wako wa kufikiria ipasavyo. Ukiokoteza maneno maneno ya kwenye blogs za chuki huko nje huwa unaziweka humu bila mwenyewe kuongeza uwezo wako wa kufikiri.
Inafaa ikuingie hamna jinsi kabila moja au mbili zinaweza kuongoza Kenya, kwa mujibu wa katiba mpya lazima ushinde kwa kushawishi nchi kwa mapana na marefu. Leo hii chama cha rais Uhuru kinaongoza kwa idadi ya wabunge, maseneta, magavana, na hata MCAs ambao zamani waliitwa madiwani.
Ili ushinde kwenye nyathifa zote hizo lazima upate uungwaji mkono maeneo mengi sana ya nchi, makabila mengi lazima yakubaliane na sera zako. Hii hapa orodha ya baadhi ya Gatuzi alizonyakua rais Uhuru nje ya mkoa wa kati GARISSA,MANDERA,WAJIR kwa Wasomali, KAJIADO, NAROK kwa Wamaasai, Pwani pia amenyakua KWALE, LAMU na pia usisahau NAIROBI amefunika, orodha ni ndefu.
Hii ramani hapa chini labda itapanua uelewa wako ili uwache kulishwa chuki za blogs
Wewe endelea kujifariji na hayo mapishi ya IEBC, mbegu ya ukabila mliyopanda haitaacha kuwatafuna.