Ndugu
dong yi
Ni ukweli usiopingika kwamba rais Uhuru ana mapungufu, lakini pia ni ukweli mtupu kwamba Raila Odinga ni mnafiki na mzandiki wa kutupwa.
Swali lako hilo Raila hawezi kulijibu bila kumumunya maneno, maana anajua siku zote umwagikaji wa damu ndio mtaji wake, tangu alipojaribu mapinduzi ya kijeshi mwaka wa 1982. Ikumbukwe leo hii afueni yetu ni kwamba hajapata nafasi ya kutumia 'Kalenjin youths' maana hao ndio walifaya mauaji makubwa ili akapata fursa ya kuwa waziri mkuu 2008.
Leo hii ameishia kutumia vijana wake wa Kijaluo maeneo machache ili wafe ndio asikilizwe, maana wakati vifo vikitokea vinaleta hisia na pia mataifa ya kigeni yanaingilia kati na kuomba apewe anachokitaka. Nina uhakika hawezi na hataki kabisa muafaka upatikane utakaohusu upigaji wa kura maana uhakika wa kushindwa upo, hivyo nia yake ni yafanyike mazungumzo ya kumpa madaraka la sivyo nchi iangamie.
Nina furaha maana Wakenya wengi hilo wameshalijua, na hizi fujo zinafanywa maeneo tu ya watu wake na sio Kenya yote. Leo hii Ukambani kule kwa naibu wake hakujawa na matatizo yoyote. Inabidi ukweli usemwe ili tuwe wapenzi wa Mungu.