Video: Ubishani ni Zanzibar ni nchi au siyo? Wenzenu upande wa Zanzibar ni Wazanzibari au Watanzania? Wasira, Rais Samia vs Tundu Lissu: Nani mkweli?

Aliyebuni jina sio Julius Kambarage Burito Nyerere au Abeid Aman Karume bali ni huyu hapa chini:
Jina la Tanzania lilibuniwa na mmoja wa wananchi walioshiriki mchakato wa kutafuta jina la nchi hii, baadaya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.Mohammed Iqbal Dar ndiye aliyebuni jina la Tanzania, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18 akiwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mzumbe.Mwandishi huyo baada ya kuonana na Mohammed Iqbal Dar akamuuliza:MWANDISHI: Uliingiaje katika shindano la kubuni jina la nchi?IQBAR DAR: Siku moja nilikuwa maktaba nikijisoma Gazeti la Tanganyika Standard ambalo siku hizi linaitwa Daily News, mikaona tangazo lililosema: "Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafahamika kama Republic of Tanganyika and Zanzibar jina likaonekana refu sana. Kwa hiyo wananchi wote mnaombwa kushiriki kwenye shindano la kupendekeza jina moja litakalozitaja nchi zote mbili yaani Tanganyika na Zanzibar."

IQBAR DAR: Nilichukua karatasi nikaandika kwanza Bismillah Raahman Rahimu hii ni kutokana na imani ya dini yangu. Baada ya hapo nikaandika jina la Tanganyika kisha nikaandika Zanzibar halafu nikaandika jina langu la Iqbal halafu nikaandika jina la Jumuiya yangu ya kidini ya Ahmadiya. Baada ya hapo nikamrudia tena MwenyeziMungu, nikamuomba anisaidie ili nipate jina zuri kutoka katika majina hayo niliyokuwa nimeandika. Baada ya hapo nilichukua herufi tatu kutoka jina la nchi ya Tanganyika yaani TAN na kwa upande wa Zanzibar nikachukua herufi tatu za mwanzo ZAN, kisha anikaunganisha nikapata jina TANZAN.

IQBAR DAR: Kabla ya kulipeleka kunakohusika serikalini nilifanya utafiti mdogo na kugundua kuwa nchi nyingi za Afrika majina yao yanaishIA na IA kwa mfano EthiopIA, ZambIA, NigerIA, TunisIA, SomalIA, GambIA, NamibIA, LiberIA, MauritanIA.
Baada ya utafiti huo nikapendekeza na kuamua kwamba jina TANZANIA ndilo litumike kuwakilisha nchi hizi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar. Kwa maana hiyo jina TANZANIA limezaliwa kutoka katika majina manne ambayo ni Tanganyika, Zanzibar, Iqbal na Ahmadiyya.

TAN-Tanganyika
ZAN-Zanzibar
IA-IQBAR AHMADIYYA
TAN-ZAN-IA
 
Uwezo wa Wasira kutumia akili umeshuka sana. Anaongea kwa kutumia nguvu bila akili. Hawezi hata kujibu hoja zaidi ya vitisho
 
Mkuu P
Yanawahusu sana Watanganyika usikwepe kwa kuwa una utambulisho halisi, sema ukweli na utakuweka huru daima. Kwanini mtu wa Zanzibar anateuliwa uongozi Tanganyika lakini wa bara hawezi kuteuliwa wala kugombea uongozi Zanzibar?
This is ridiculous to argue with the intellectuals
 
Unahitaji elimu ya uraia kuhusu haki za Mtanzania, kila Mzanzibari kwanza ni Mtanzania ndipo kisha ni Mzanzibari. Lakini sio kila Mtanzania ni Mzanzibari!. Haki za Zanzibar ni kwa Wanzanzibari wakaazi pekee!.

Ukioa mke, anakuja kwako, na anakuja kwenu, kwako kunakuwa kwake, na kwenu ni kwake, lakini kwao ni ukweni ni kwao tuu, ukweni kwa mkeo sio kwako!. Zanzibar ni ukweni!. Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?
P
 
Sihitaji elimu yako gushi ya uraia wakati nina akili timamu, nimesoma na ni uwezo wa kuchanganua mambo 'empirically' halafu unaniletea nadharia za siasa uchwara bila uhalisia (Utopian) hapa.

1. Mme ni nani kati ya Tanganyika na Zanzibar?

2. Mke ni yupi kati ya Tanganyika na Zanzibar?

Je, wajua kwamba

1. Tanganyika inawakilishwa na mnyama Simba na wala sio Twiga?

2. Je wajua Zanzibar inawakilishwa mnyama Mbuzi na chui na sio Pweza na Mwani?
 
Ndoa ya muungano sio ndoa za jinsia, ni ndoa ya two equal partners wenye haki sawa and equal status.
P
 
🤔🤔🤔⁉⁉⁉
 
Ndoa ya muungano sio ndoa za jinsia, ni ndoa ya two equal partners wenye haki sawa and equal status.
P
P, umechokonoa kitu usichojua madhara yake

Taja hapa ni nani mme au mke kati ya Tanganyika na Zanzibar kwa mwenziwe?

Usizunguke kama nguchiro kwa kuwianisha hadhi za mamlaka ya usawa usiokuwepo. Tusiwe na mawazo tegemezi yaliyotekwa na kikundi fulani (elites) dhidi ya watu wasiojitambua (lumpen)
 

Mwanasheria Pascal Mayalla naona umeamua kupambana kwa kupiga mayowe badala ya kuyatazama mambo ktk jicho pevu la kisheria..

Kama umefikia hatua ya kutamka "tutaulinda muungano huu kwa gharama zozote", ila ujue kuwa tupo tutakaosema "huu muungano tutaufutilia mbali kwa gharama zozote".

Kukiwa na confrontation ya dizaini hii kati ya wawili katika ndoa, unadhani kutatokea nini kwa kusigana huku badala ya kupatana kwa kutatua kasoro za ndoa yetu?

Umeulinganisha muungano kama ndoa ya mume na mke, na kwamba, kusisitiza kuwa wanandoa huwa hawaachani. Lakini hii ina ukweli wowote?kweli?

Mr Pascal Mayalla ndoa huvunjika. Hata hii inaweza kuvunjika na kama hao wenzako huko wana mawazo kama yako, basi itavunjika haraka sana..
 
1. Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye uraia mmoja tuu wa JMT. Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT.
2. Wananchi wa Zanzibar ni Watanzania ila pia ni wakaazi wa Zanzibar. Ukaazi sio uraia.
P
Paschal leo umeandika hisia au halisia? Kwa hiyo unamaanisha Mzanzibar ni uraia batili?
 
Unataka maneno ya wanasiasa au unataka Katiba ambazo ndio miongozo?
Katiba ya Zanzibar kwenye Preamble inasemaje?
Katiba ya Tanganyika inasemaje?
 
Paschal leo umeandika hisia au halisia? Kwa hiyo unamaanisha Mzanzibar ni uraia batili?
Sio ubatili, hakuna raia wa Zanzibar kwasababu Zanzibar sio nchi, haina raia, nchi ni Tanzania na uraia ni mmoja tuu, uraia wa Tanzania.

Ila Zanzibar ni eneo halali lenye utawala wake wa ndani na eneo hilo lina wakaazi, hivyo kile kitambulisho cha ukaazi wa Zanzibar ni kitambulisho cha ukaazi wa eneo la Zanzibar na sio kitambulisho cha uraia wa Zanzibar, hakuna raia wa Zanzibar, raia wote ni raia wa Tanzania na wana haki zote za uraia sawa sawa ikiwemo kumiliki ardhi na ajira ndani ya JMT!.
P
 
Muungano ni imara kwa sababu inatumika nguvu ya dola . Upinzani ulikuwa Zanzibar tu ,lakini kidogo kidogo wa Tanganyika mnaanza kujitambua ingawa wenye njaa na walafi mko wengi mnaojipendekeza kwa wenye Muungano
 
Wakati wa Karume Sr. Ukifika 18yrs. Ilikuwa lazima uchukuwe id inaitwa Kadi ya Uraia
Hiyo ilithibitisha Uraia wako. Na ilikuwa hupati hata kununua nguo dukani Kama huna hiyo Kadi . Hizi Kadi ziliondoka baada kuuliwa Karume. Lakini bila Kadi Wazanzibari tunajuana.
 
Sasa wewe huu ni muungano gani?. Zanzibar si wana rais wao. Vile vile Tanganyika wapate rais wao. Harafu kuwe na rais wa muungano wa nchi zote mbili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…