Usengerema mtupu.
CCM imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutumia vyema mtaji wake wa upumbavu na ufukara wa wananchi wa Tz kuweza kujijengea mizizi.
Kwa akili ya kawaida ingekuwa kuna uelewa na kutokuwepo na dhiki kwa wananchi, hakuna mtu mwenye akili timamu angekubali kujidhalilisha kama hivyo kwa kujijaza matope mwilini ikiwa viongozi wamo kwenye magari na kumbi zenye Ac.
Ingekuwa kusherehekea ni kujipaka matope basi angejipaka Samia na Wassira kwanza, kama viongozi wa juu ilipaswa wawe na furaha zaidi.
Hapo ukiuliza hao kina Lucas Mwashambwa waliojipaka matope wamepewea elfu 5 kila mmoja ili wajidhalilishe ila ndani ya nafsi zao wanajua fika kuwa hakuna la maana walilofanyiwa na CCM.