VIdeo: Wabunge wa Marekani waandamana hadi mbele ya jengo la USAID wakitaka misaada irudishwe haraka, wataka Elon adhibitiwe!

VIdeo: Wabunge wa Marekani waandamana hadi mbele ya jengo la USAID wakitaka misaada irudishwe haraka, wataka Elon adhibitiwe!

Wal
Tayari zimeshafungwa, wafanyakazi wapo majumbani sasa
Walikuwa wanatudinyia madem zetu sasa zam Yao. Sisi laki mbili zetu bado zipo palepale. Na kibaya zaidi haya mashirika hayana mpango wa kumuwekea mtu akiba za kustaafu wanakupa kila kitu utajua mwenyewe huko. Tujiandae kununua mali zao kwa bei ya kutupwa kwa wale ambao walijisahau
 
😁😁😁😁, taratibu mkuu.. Waliowengi wamejiunga na grade ya Taifa.. Kula kwa umakini sana
 
Wakuu,

Huko nchini Marekani, viongozi na baadhi ya wabunge wameandamana nje ya jengo la USAID wakitaka shirika hilo lirudishwe na misaada irudi haraka sana.

Jamii Raskin ambaye ni mbunge kutoka jimbo la Maryland aliongozana na wabunge wengine wakitaka shirika hilo LIRUDISHWE na Elon Musk asijihusishe na shughuli zozote za kiserikali.

"Elon Musk hukuitengeneza USAID, Marekani kupitia bunge ilifanya hivyo kwa ajili ya Wamarekani. Hana nguvu ya kuiharibu (USAID) na nani ataenda kumdhibiti (Elon)? Ni sisi hapa. Hatuna mhimili wa nne wa serikali unaoitwa Elon Musk"

===================

Elon Musk sio mbunge wala hajachaguliwa na wananchi wa Marekani kwanini Trump anampa mamlaka makubwa sana na hajachaguliwa wala kupitishwa na bunge?

Trump na Elon inaelekea wameshindilia Chumvi nyingi kwenye Kidonda...Mafisadi hawaamini
 
Back
Top Bottom